Maajabu ya Dunia!

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
3,140
5,035
Karibu tupate kufahamu machache kutoka kwa wenzetu huko!

1. New York, Marekani
Jiji lla New York lilikuwa na utamaduni wa ajabu kidogo haswa katika miaka ya 1920s, kwani tarehe moja mwezi Mei ambayo kwa sasa tunaadhimisha sikukuu ya Wafanyakazi basi wapo ilikuwa ni siku ya kuhama maarufu kama Moving Day ndani ya Jiji la New York.

shutterstock_248799484-scaled.jpg
Kama ulikuwa na fikra za kuhama makazi basi ilikubidi kusubiria mpaka tarehe moja mwezi Mei ndo uhame, na watu wote walihama na kuhamia makazi mapya ndani ya siku moja. Kadri jiji lilivyokuwa likipata watu na kuongezeka basi siku hii ikawa inazidiwa kwani mitaa ilikuwa na watu ambao ndo walikuwa kwenye pilikapilika za kuhama. Ila kwa sasa wakazi wa New York wanaweza kuhama siku yoyote ile katika kalenda.

2. London, Uingereza
Madereva Taxi ndani ya Jiji la London wana kazi ya ziada ya kusoma na kuelewa majina yote ya mitaa ya London pia wanahitajika kuelewa vyema ramani ya Jiji lote na hii huwachukua mpaka miaka minne huku pia wakitakiwa kufuzu mitihani ili kuona uwezo wao wa kuielewa London. Na baada ya mitihani hiyo ndipo wanapoweza kupata leseni ya kuzunguka mitaa ya London.
study-in-london-1068x641.jpg

Iwe ni Abbey Road, au Oxford Street, Regent Street kitaalamu wanatakiwa kuzielewa njia maarufu zaidi ya 320 ambayo imesambaa kwenye mitaa zaidi ya 25,000, huku pia wakifahamu alama za kila mitaa hiyo, kama viwanja na sanamu maarufu, yote haya yakae kichwani na endapo mtu akiwa hajui anapokwenda basi akielezea kuwa mtaa huo una sifa ipi basi dereva aweze kuelewa ni mtaa gani.

3. Berlin, Ujerumani​
2d8fhj1.jpg

Jiji la Berlin ndo linaongoza na kufika nambari moja kwa kuwa na makumbusho nyingi duniani, zaidi ya makumbusho 170 ndani ya Jiji moja tu, Ajabu sana! Berlin ina makumbusho nyingi kuliko siku ambazo inapata mvua! Kuna makumbusho ya historia, makumbusho za kisayansi, makumbusho za chakula na vinywaji kama pombe. Kumbuka kuna majiji yana makumbusho moja au mbili tu, ila Berlin ina makumbusho zaidi ya 170.

4. Tokyo, Japani​
img_access_02.jpg

Jiji la Tokyo ndio jiji ambalo njia zake za chini ya ardhi pamoja na mifumo ya treni ina miundombinu mikubwa
na yenye kuhudumia watu wengi pamoja na kuwa busy kila wakati, sasa kwenye nyakati haswa za asubuhi na
jioni wakati ambao watu wengi wanakuwa wamejaa wakisubiria treni katika vituo.
8e9d13b8e5f4c97c518832af1bc95724.jpg

Hivyo wamepata kuajiriwa watu ambao wanaitwa Oshiya ama wasukumaji, ambao hawa kazi yao ni moja tu, wanajichanganya na kuwa kama vile abiria ila wakati tu milango ya treni imefunguka basi Oshiya wanawasukuma watu wapate kuingia ndani ya treni. Tunatakiwa kuwa na kina Oshiya wengi kwenye mwendokasi.

5. Los Angeles, Marekani​
Hollywood_Sign_(Zuschnitt).jpg

Lile bango kubwa la HOLLYWOOD ambalo linatia nakshi jiji la Los Angeles lilianza kutumika mwaka 1923 ila lilikuwa likisomeka kama HOLLYWOODLAND na lilikuwa ni tangazo la kipindi kipya ambacho nyumba na makazi mapya yatakwenda kujengwa katika eneo la Hollywood.
hollywoodland.jpg

Sasa mwaka 1949 idara ya Los Angeles Parks and Recreation ilitaka kuondoa bango hili, ila mamlaka ya Jiji la Los Angeles ilipinga na kuamua kuondoa neno LAND tu na kubakiza neno HOLLYWOOD.

6. Seoul, Korea ya Kusini
Jiji la Seoul ndio kitovu cha teknolojia na uvumbuzi duniani, ndani ya Korea ya Kusini ndipo kwenye intaneti yenye kasi kubwa zaidi duniani! Kasi ya zaidi ya megabits 26.1 kwa sekunde moja, pia Korea ya Kusini ndo kwenye upatikanaji mkubwa na ulio bora wa mitandao kwa kiwango cha 4G.
old-fortress-gate-with-light-trails-at-downtown-455242307-58dea6143df78c5162e1ff3d.jpg

Kama unataka kuingia mtandaoni basi ukiwa Korea ya Kusini, uwezo wa kupata mitandao ni kwa asilimia zaidi ya 95!

7. Barcelona, Uhispania
Umewahi kusikia kuhusu Kanisa la Sagrada Familia ambalo lipo katika Jiji la Barcelona? Basi huu ndo ujenzi ambao umechukua muda mrefu kukamilika zaidi duniani, kuliko hata ujenzi wa Great Pyramid of Giza ambao zipo huko Misri.
interior.jpg

Ujenzi wa Sagrada Familia ulianza mwaka 1882 na mpaka unategemewa kukamilika mwaka 2026, yaani Sagrada Familia inajengwa kwa zaidi ya miaka 144!

8. Cape Town, Afrika Kusini​
cape-town-aerial-view-greenpoint-stadium.jpg

Jiji la Cape Town ndo jiji ambalo linatoa huduma za kiwango cha juu kwa watalii, na wapo wale ambao hupenda kutazama ndege aina ya penguins, sasa ukiwa Cape Town kuna penguins wanaoitwa African penguins zaidi ya 2000 ambao wengi wao huonekana kwenye fukwe za Boulder beach.
animals_hero_penguin_02_1.jpg

Lakini African penguins wamekuwa eneo hilo miaka kati ya 30 mpaka 40 iliyopita, na hii ni sababu ya watu kufanya uvuvi mkubwa wa dagaa kwa kiasi kikubwa kati ya miaka ya 1960 mpaka 1970 na hivyo kuwafanya kukosa chakula cha kutosha na kuondoka kwenye mazingira yao ya kuzaliana.

9. Lisbon, Ureno​
A-Brief-History-of-Greece-1440-x-675-900x420.jpg

Ukiuliza majiji ya zamani zaidi duniani, najua utasema kuwa kuna Athens pamoja na Rome ila amini usiamini
Lisbon ni mji mkongwe na ulikuwepo toka miaka 1200 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo na ndo mji wa pili mkongwe ndani ya Ulaya nyuma ya Athens.
lisbon-portugal-LISBONTG0521-c933a0fb669647619fa580f6c602c4c8.jpg

Lisbon una miaka zaidi ya mia nne mbele ya Jiji la Rome, na moja ya kitu ambacho kinaipa sifa sana Lisbon ni mara baada ya kupigwa na tetemeko la ardhi mwaka 1775 ila bado Jiji likajijenga na kuwa zuri zaidi.

10. Shanghai, Uchina
Kipindi ambacho Uchina ilifungua rasmi mifumo yake ya safari za reli kwa mwendokasi kati ya Majiji mawili ya Shanghai na Beijing, majiji mawili ambayo yameibeba Uchina katika biashara, uchumi na siasa.
istockphoto-665298978-612x612.jpg

Basi wafanyakazi wa reli walifundishwa kutoa tabasamu pana mithili ya ndegere yaani ilifikia sehemu walitakiwa kuonesha meno nane wakiwa na tabasamu ama nanili akiwa amepata ofa ya bia (Utani kidogo), ila jambo hili halikuwa rahisi kama wengi wanavyodhani hivyo wengine walitumia vijiti kushikiria taya yao wakati wa mafunzo! Tabasamu mpaka jino la mwisho ama kibarua kiote nyasi.

11. Milan, Italia
Ukipata nafasi ya kufika kwenye Jiji la Milan basi ulizia kuhusu utamaduni wa Aperitivo, ambapo huu ni utamaduni wa zamani ambao mpaka leo bado upo unaendela kuenziwa na wazawa wa Milan, Aperitivo ni mfululizo wa vinywaji na chakula ambacho hupewa mtu ili apate hamu ya kula na wakati mwingine kumuandaa kwa chakula ambacho kipo jikoni kinakaribia kufika mezani.
Article-How-to-Italian-Aperitivo-Spread-Spritz-Cocktail-Recipe.jpg

Aperitivo inaweza kuwa ni nyama ya kuchoma, au tambi na wakati mwingine vipande vichache vya pizza au kachumbari za matunda, lakini upande wa vinywaji basi hakuna idadi kwani vinywaji hukuweka sawa wewe na tumbo ili kujiandaa kupokea chakula. Aperitivo huanza kuanzia majira ya saa 12 jioni ama saa 1 jioni na inakoma majira ya saa 3 usiku! Hapa kina Fulani mtashiba kwenye aperitivo tu kabla hata chakula hakijafika mezani.

12. Tokyo, Japani
Ndani ya Jiji la Tokyo kuna vyoo ambavyo vimepewa jina la smart-toilets, vyoo ambavyo vitakupatia nafasi ya kujisaidia vyema kuendana na mahitaji yao, kuna vyoo ambavyo vina vitambaa laini, sufi na umaridadi wa kila aina kuendana na mahitaji ya mtu.
merlin_175888860_78381607-2443-4078-b4c7-c9c7a7921089-superJumbo.jpg

Vipo vyoo ambavyo vinafanya kazi ya kukusafisha wewe pamoja na kuondoa uchafu wote, ukitaka maji ya moto ama vuguvugu au kiti cha kukalia kiwe na joto (kazi ni kwako!)

13. Paris, Ufaransa
Kwa sababu ya namna ambavyo Jiji la Paris linavyochorwa na vyombo vya habari, watu wengi hutumbukia kwenye fikra kuwa Paris ni Jiji nzuri na rafiki kwa kila mtu na wengine huona ni kama mbingu ya dunia, kisanga kinakuja kwa watalii ambao baada ya kufika na kukutana na uhalisia wanatambua kuwa sio kweli.
france.jpg

Vyakula ni gharama na maisha sio kama yalivyo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, basi watu wengi huishi kuwa na msongo wa mawazo, na wakati mwingine hupata hasira na majuto ambayo wanasaikolojia wamekuja kuipatia hali hii jina la the Paris Syndrome.

14. Venice, Italia
Kila mwaka Jiji la Venice hupokea watalii zaidi ya milioni 18, yaani watalii zaidi ya 60,000 kila siku! Hapa ni Venice tu yaani sehemu ya Italia inapokea watalii milioni 18, na idadi hii inazidi idadi ya wakazi wa Venice.
190615084315-venice-overcrowding-1.jpg

Hali hii inatishia kuharibu na kuondoa kabsa uwepo wa wazawa wa Venice kutokana na kupanda kwa gharama za huduma na bidhaa haswa chakula. Baadhi ya wataalamu wa uchumi wameonesha hofu zao kuwa mpaka kufikia mwaka 2030 basi Venice itakuwa haina wazawa tena na itabadilika na kuwa Jiji la kivutio tu.

15. Stockholm, Sweden​
fossile-free-buses-sweden.jpg

Ukiwa ndani ya Jiji la Stockholm na unasafiri na mtoto mdogo kwenye kitorori cha kubebea wato basi hautolipa pesa ya nauli katika basi. Kama naona wabongo tunavyomezea mate hii ofa! watu wataomba watoto kwa majirani waende nao!

16. Amsterdam, Uholanzi​
MIT_Stolen-Bikes-01-press.jpg

Jiji la Amsterdam lina jumla ya baiskeli laki nane na elfu themanini huku pia likiwa na wakazi laki nane tu, hii ina maana ya kwamba Amsterdam ina baiskeli nyingi kuliko watu.

17. Atlanta, Marekani​
Canopy-ATL-illuminated-sky_-copy-900x500.jpg

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hartsfield-Jackson International Airport uliopo kwenye Jiji la Atlanta Marekani ndo uwanja unaoshika nambari moja kwa kuwa na harakati nyingi zaidi duniani, kituo cha abiria ndani ya Hartsfield-Jackson International Airport kina ukubwa sawa na viwanja vya mpira wa miguu zaidi ya 45! Uwanja wa hapo kwenu una ukubwa gani au nikae kimya?

18. Mumbai, India​
mumbaitrainjfif.jpg

Usafiri wa reli ndo usafiri ambao umebeba maisha ya raia wa India, basi tambua kuwa usafiri wa reli ndani
ya India hubeba watu zaidi ya milioni sita kila siku, hapo ni zaidi ya idadi ya wakazi wote wa nchi ya Finland.​

WEKA NA YAKO HAPA!
 

Attachments

  • image_readtop_2020_1106605_16038662024409350.jpg
    image_readtop_2020_1106605_16038662024409350.jpg
    56.3 KB · Views: 17
Back
Top Bottom