Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 45,796
- 65,052
Ukifuatilia mitandao ya kijamii utagundua CHADEMA ndicho chama chenye wafuasi au wapambe wengi sana katika mitandao ya kijamii nchini, katika hili utakosea sana ukifikiri uwakilishi mitandaoni unawakilisha uhalisia nje ya mitandao( kwa ground).
Maandamano yakiitishwa na viongozi wa CHADEMA huwezi kuwaona wafuasi wa chama waliojaa tele mitandaoni.
Viongozi wa CHADEMA wakikamatwa, wakipotea, wakipigwa, wakilazwa magereza, wakiuwawa huwezi kuona reaction yoyote ya wafuasi wa CHADEMA nje ya mitandao.
Wagombea wao wakienguliwa katika chaguzi au wakinyang'angwa ushindi hakuna chochote cha maana wanaweza kufanya.
Wameshindwa kumchangia Lissu buku buku anunue vietee lakini wanataka V8 yake iliyopigwa risasi iwekwe makumbusho ya CHADEMA!
Hata hili la sasa la kikundi fulani cha mtandaoni kutokwa na povu kuhusu Mbowe bila shaka inaweza kuwa ni upepo tu wa mitandaoni ila kwa wanachama halisi hali ni tofauti sana kwa ground, ni wakati sasa keyboard warriors wapuuzwe.