Maafisa wa Posta Tanzania wakutwa na kesi ya kujibu kuhusu kusafirisha Dawa za Kulevya

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,819
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewakuta na kesi ya kujibu, maofisa watatu wa ulinzi wa Shirika la Posta Tanzania, wanaokabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine na bangi.

Maofisa hao ni George Mwamgabe, Sima Ngaiza na dereva wa Shirika hilo Abdulrahman Msimu.

Washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi gram 124.55 na heroine gramu 1.55, kosa walilodaiwa kulitenda Agosti, 2018 katika ofisi za Posta, Ilala jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutumia Shirika la Posta, kusafirisha dawa hizo zikiwa katika vifurushi kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro, wakati wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Mwamgabe na wenzake wamekutwa na kesi ya kujibu leo, Agosti Mosi, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Richard Kabate, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya uamuzi iwapo washtakiwa wanakesi ya kujibu au laa.

Hakimu Kabate amesema amepitia ushahidi wa mashahidi 18 na vielelezo tisa, ambapo kupitia ushauud huo Mahakama hiyo imewakuta na kesi ya kujibu.

Hakimu amesema, kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani kuna haja ya washitakiwa hao kuieleza mahakama ushahidi wao kulingana na mashitaka yanayowakabili.

"Mahakama imewakuta na kesi ya kujibu, baada ya kupitia mashahidi 18 na vielelezo tisa, hivyo washtakiwa wanatakiwa kuanza kujitetea" amesema Hakimu Kabate.

Hata hivyo, washtakiwa hao wamedai kuwa watajitetea kwa kiapo na watakuwa na mashahidi pamoja na vielelezo.

Washtakiwa baada ya kueleza hayo, Hakimu Kabate ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14, 2023 ambapo washtakiwa hao wataanza kujitetea.

Awali, kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, wakili wa Sarikali Ashura Mnzava amedai kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi na upande wa mashtaka upo tayari kusikiliza.

MWANANCHI
 
Hii habari ya Muda sana na Watuhumiwa wa kesi husika walishachukulia hatua za kinidhamu.
Hili shirika la Posta kwa sasa limeimarisha sana usalama wa ukaguzi wa vifurushi na mizigo katika ofisi zake zote kwa kuongeza Scanners na CCTV Camera nimeshuhudia mara kadhaa nilipokwenda kutuma mizigo yangu katika Ofisi zao.

Hongera sana Postamasta Mkuu wa Shirika hili ndg. Mbodo kwa Mageuzi makubwa uliyoyafanya.
 
Taarifa kama hii haina tija kwa jamii, Kwa mageuzi haya ya Shirika la Posta hata uwe na 0.000001gm ya Dawa Za Kulevya hupenyi popote pale!!!!

Tuache kuzua taharuki zisizo na msingi kwa shirika linalifanya vizuri kama Posta, taarifa ya 2018 almost 5years now na wahusika walishachukuliwa hatua. Tuachane na hizi habari tuangalie mazuri ya shirika hili hasa kwa kipindi hiki.

Shirika hili limekua msaada mkubwa sana kwetu hasa wafanyabiashara.
 
Back
Top Bottom