A
Anonymous
Guest
Sisi wakazi wa Matuga, Kibaha Vijijini tuna changamoto ya kusumbuliwa na Maafisa wa Halmashauri ya Kibaha Mji, wapo katika mchakato wa kutupora ardhi yetu kiasi cha kutumia Askari Polisi na Mgambo kutekeleza nia yao hiyo.
Hawa Watu wa Halmashauri ya Kibaha Mji huwa wanakuja kwenye makazi na mashamba yetu nyakati za usiku na wakati mwingine mchana kwa lengo la kupima viwanja.
Ikifika asubuhi wanawaleta watu na kuwagawia maeneo hayo huku wakiwa na Askari mwenye bastola, nimeambatanisha picha ya moja ya matukio ambayo inamuonesha jamaa mwenye T-shirt ya njano ambaye ndiye askari wanayemtumia hapo Halmashauri mara kadhaa.
Maafisa wa Serikali wakiwa na Askari.
Moja ya gari la Halmashauri ya Kibaha Mji lililofika Matuga likiwa na maafisa waliokuja kutoa vitisho kwetu.
Sisi zaidi ya Wananchi 400 tulipata kadhia ya kusikitisha mnamo Februari 2, 2023, tulibomolewa makazi yetu chini ya usimamizi wa Askari na Maafisa wa Serikali pasipokuwa na taarifa yoyote ya awali juu ya ubomoaji huo.
Wabomoaji walifika tu siku hiyo wakaanza kuvunja na kututaka tutoe vitu ndani au tutoke, la sivyo wanavunja bila kujali nani yupo ndani.
Tukaenda kushtaki Mahakama Kuu Divisioni ya Ardhi, Februari 6, 2023 tukafungua kesi na Juni 30, 2023 hukumu ikatolea kuwa tumevunjiwa makazi yetu kinyume cha Sheria.
Kuanzia hukumu ilipotoka tumekuwa tukipata usumbufu kutoka kwa maafisa hao wanaotutishia usalama wetu.
Kuna wakati wanakuja na watu wanaodai wamebomolewa nyumba maeneo ya Mitamba na Loliondo (Kibaha), hivyo wanakuja kuwapatia maeneo huku kwetu kinguvu.
Wananchi wa Matuga
Nyumba zilizobomolewa lakini baada ya muda Mahakama ikatoa hukumu kuwa ubomoaji ulifanyika kimakosa.
Mkuu wa Mkoa anajua hili jambo lakini hajatuma msada wowote, Mkuu wa Wilaya naye aliwahi kutuambia kuwa kama tunaona hatuko salama tufunge matairi nyumba zetu tuhame.
Tunamuomba Waziri Jerry Silaa na Rais Samia Suluhu Hassan watusaidie, tumekuwa kama wakimbizi ndani ya Nchi yetu wenyewe.
Viongozi wa Kibaha Mji wajue kuwa hii Nchi ni ya ketu sote na inaongozwa na Sheria, wao hawapo juu ya Sheria. Haki tuliyoipata Mahakama Kuu inatakiwa kuheshimiwa.
Msingi wa nyumba uliobomolewa wakati wa bomoabomoa