Maafisa Polisi Jamii wapewa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kujua majukumu yao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,733
13,488
2.jpg

Jeshi la Polisi limetoa mafunzo ya siku moja kwa Maafisa Polisi Jamii na Polisi Kata kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam pamoja na wengine kutoka Kibaha na Mkuranga.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP David Misime amesema mafunzo yamefanyika baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura kupanga askari wakaguzi katika kata zote Nchini.

Amesema Tanzania Bara kuna Kata 3,956 wakati Zanzibar kuna Shehia 288, hivyo jumla ya wakaguzi waliopangwa kwenye Kata ni 2,372 na askari wa kawaida ni 1,584, wakati upande wa Zanzibar, Shehia zote zimepangwa Wakaguzi na Askari Kata.
3.jpg

Ameongeza kuwa baada ya kuwapanga Maafisa hao kinachofanyika ni kuwajengea uwezo wa kwenda kutekeleza majukumu ya Polisi Kata katika maeneo yao ambayo wanatakiwa kuelimisha Wananchi wa kada zote kuanzia ngazi ya Shule ya Msingi

Ameeleza kuwa Polisi Kata wanatakiwa kuyatekeleza majukumu yao kisha kutoa elimu katika Jamii ili kujenga urafiki na kuwa na urahisi wa kubaini uhalifu kwenye ngazi za Kata.
5.jpg

SACP Misime

SACP Misime amesema elimu nyingine iliyotolewa ni kuhusiana na falsafa ya Polisi Jamii jinsi gani Polisi wanavyoweza kushirikiana na jamii pamoja na kujua changamoto mbalimbali za uhalifu kwenye jamii.
 
Back
Top Bottom