MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 376
- 639
Jeshi la M23(siliiti kundi tena, kwa walivyofanya, wana hadhi ya kuitwa wanajeshi), huko Kivu kusini, limezitaka taasisi zote za kiserikali kuendelea kutoa huduma kama kawaida.
Kuna taasisi ambazo, wafanyakazi walikimbia na kwenda mikoa au nchi jirani, wengine wakienda Kinshasa jijini. Baada tu ya kufika Bukavu, wafanyakazi wa ofisi za uhamiaji upande wa Congo walikuwa wameshakimbia na kuacha ofisi. Japo huduma zilikuwa hazitolewi, lakinin wenye hati za kusafiria, hawakuzuwiliwa kuingia nchini Rwanda au kupokelewa watokapo Rwanda, japo upande huo walikuwa hawagongewi mhuri ikiwa wanatoka au wanaingia.
AFC/M23 imejitahidi kuhakikisha raia wanapata huduma haraka iwezekanavyo,katika nyanja mbali mbali. Watoa huduma wengi, mjini Bukavu, baada ya kuona hali ilivyokuwa Goma, hawakuwa na wasiwasi, na walipoitwa, waliokuwa karibu wote walirejea maofisini kwao.
Kasoro Benki tu,ambapo badhi ya viongozi wanajadiliana uwezekano wa kutoa huduma hiyo. Pia, tofauti na mji wa Goma, serikali ilipokuwa imekata huduma za maji na umeme, Bukavu haikuwa hivo. Pia huduma za mtandao ziliendelea, kasoro tu mitandao ya kijamii.
Mpaka sasa, watoa huduma wote walishaahidiwa kupokea mishahara yao kama kawaida, huku wa kwanza kupewa stahiki zao, wakiwa wanajeshi waliokuwa wakipigana upande wa serikali. Kwa sasa, watakuwa wakilipwa mishahara yao kila mwezi,kama waajiliwa wote.
Taarifa ambazo pia binafsi sijadhibitisha, ni kwamba punde tu watakapokamilisha zoezi lao, mishahara yao itarekebishwa, na familia zao kupewa vipaumbele katika mambo mbali mbali, yakiwemo huduma za afya, shule na maisha ya kawaida.