Lyrical and naturally gifted African (Langa) Mengisani Kileo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,172
RAFIKI WA KWELI;
LYRICAL AND NATURALLY GIFTED AFRICAN (LANGA) MENGISENI KILEO
1. "HAKUNA MC ANAYENISHINDA KWA HIP HOP "
2. " HIP HOP NI UKWELI NA UWAZI, KUKU KAPANDA BAISKELI HAIKUSHANGAZI"
3. "HIP HOP ND'O MAISHA ASIJE MTU KUBABAISHA"
4. " USISUBIRI MPAKA NIFE ND'O UKUBALI I'M THE BEST"
5. " KICHWANI N'NA NYIMBO NYINGI KAMA MP 3"
6. " NAPENDWA NA WACHACHE, NACHUKIWA NA WENGI ILA NAHESHIMIWA NA WOTE UWE UNAPENDA AMA HUPENDI"
7. "KIINGEREZA BILA HELA SAWA NA KUPIGA KELELE"
8. "BADALA YA KUHUKUMU KAMA VILE TUPO COURT, NUNUA KAZI ZANGU, SON ONESHA SUPPORT"
9. "REAL LOVE NI ADIMU KAMA MENO YA TEMBO"
10. "GOD MADE MONEY
MONEY MADE MAN MAD"
A true billingual, "naflow kwa KIINGEREZA, naflow kwa KISWAHILI/ Hata Jigga haniwezi, mi naflow kwa lugha mbili."

Mtetezi halisi aliyeiishi HIP HOP maisha yake yote. Kaisikilize HIP HOP.

Hata baada ya kuvunjika kwa COCACOLA POP- STARS (WAKILISHA) iliyotamba na ngoma kama: HOI na KISWANGLISH, akabaki na Witness na kutoa NO CHORUS kama dongo kwa Sara lakini pia kila mmoja alipopita kimpango wake, alisimama na game yake.

Kutumbukia kwenye dawa za kulevya kulimfanya apitiwe na Jay Moe kwenye JIPANGE, hakukaa kimya akamjibu:

" Amani kwa Voda MILIONEA, mwambie mdogo wako aache ushoga na umbeya." Ishu ikawa ishu kweli lakini baada ya kuachana na uraibu, Langa akalamba matapishi yake na kusema; " Amani kwa Kaka Voda MILIONEA, mwambie MOE nimeacha poda pia sili mmea"

Japo ugomvi wao uliisha lakini Moe amenukuliwa mara kadhaa akisema anaumia kila akikumbuka sintofahamu iliyokuwepo baina yake na Langa.
Aliwahi kuwa katika vita baridi na Fid, ambaye alimshirikisha kwenye NI HAYO TU na CHAGUA MOJA.

Fid Q akamwalika Langa kwenye kipindi chake cha FIDSTYLE FRIDAY na kuonesha kuwa hakukuwa na shida baina yao.

Miaka ikaenda, LANGA akatoa RAFIKI WA KWELI, mkono wa Majani, mara Fid naye akaibuka na SIHITAJI MARAFIKI, pale TONGWE. Hii ilizua maneno kwa baadhi ya watu.

Mzalendo na mwana halisi wa Afrika, sikiliza NINAKOTOKA FT NECESSARY NOISE.

Inasemekana Langa alikuwa miongoni mwa "WACHOYO WA KOLABO" na hata ile NINAPOSIMAMA, Chid alimchana akiwa booth kwa Lamar na Dunga na kusema, sikubali, mtu gani unafanya ngoma mwenyewe tu, hii, tunafanya wote na ndipo akaja na " ONE TO ONE... NA AMBII KA REFARII, RECORD HII YA 41"
Oyaa!! Hii ilikuwa kamba au ndivyo ilivyokuwa??? Niliipata kwa mwanangu mmoja hivi pindi hiyo.

1. FIKRA POTOFU - SALU T
2. NAJUA UNANIKUBALI - MANSU LEE
3. GANGSTAR
4. HIP HOP
5. NINAKOTOKA
6. NINAPOSIMAMA
7. MATAWI YA JUU
8. PIPI YA KIJITI
10. HOI
11. LOOSE YA' HEAD - BONGO RECS
12. KISWANGLISH
13. NO CHORUS
14. PESA FT JIDE
15. KAMA BOSS FT TID
16. WAZAZI
17. RAFIKI WA KWELI
18. NI HAYO TU
19. CHAGUA MOJA
20. MTIMANYONGO - SHAA (SARA)
Unamkumbuka zaidi kwa ngoma gani?
Ngoma gani zimesahaulika kwenye orodha?
Ameacha alama gani ambayo inafanya usiusahau uwepo wake kwenye game??
YOUR LIFE WILL BE FOREVER CHERISHED
THANKS FOR THE MUSIC, BRO!!
PEACE!!!
1678859884713.jpeg

1678859902695.jpeg

1678859913179.jpeg
 
Kwenye izo nyimbo ya Rafiki wa kweli Langa na sihitaji marafik umechanganya, Fid Q ndio alianza kutoa sihitaj marafik mwaka 2012 miezi ya mwanzo(3-6) ila Langa na Rafiki wa kweli aliitoa 2013 Kwenye mwezi Wa5 mwshon kipindi cha msiba wa Ngwair na Aliojiwa Friday Night Live EATV na alielezea kuguswa kwake na msiba wa Ngwea ila Wiki mbili mbele na Yeye Langa Akafariki, Pumzika kwa Amani mtoto wa Kishua Langa Kileo
 
MBona Hujizumgumzia matawi ya juu???
Hiyo ndo Ngoma iliyonifanya nikaanza kumfatilia Sana Langa..

Kwangu Langa ni zaidi ya Legend coz kwenye kila Ngoma yake lazima alikua anakuacha quote ambayo utanitumia tu maishani...
Mfano kwenye hiyo Ngoma ya matawi ya juu kuna mstari anasema.. "kama Una familia ni Bora usiniige Mimi, hukawii kuuza nyumba usipokua Makini..."
Matawi ya juu ni Ngoma inayozungumzia starehe na anasa za juu. Kumbuka Langa alikua mtoto ya kishua Kasoma pale Loyola sec. Mama yake alikua barozi huko abroad so kwao hela ya kubadili nguo na mboga haikua Stori.. ingawaje Langa alikua mtu royal Sana na aliyechanganyikana Sana na masela hivo aliielewa Sana tabu na adha wanazopitia watu wenye Maisha ya dhiki mfano vijana wanaokaa ghetto na alipenda kua nao karibu yeye aliwaita Askari wake. Tuki-refer hiyo Ngoma ya matawi ya juu kuna mstari anasema "ukinicheki msafi niguse uone Moto, sitokei masaki natokea king'oko!...

Langa alikua msanii aliyekamilika kila idara kuanzia rap style, sauti, vina, punchline, na pia alikua so loyal kuongea matatizo ya mtaani kabisa...
"Rais wa ghetto, mtetezi wa wanyonge mwakilishi wa mitaa Kwa wenye shida na njaa..." Ndivo alivoanza kuchana kwenye Ngoma ya "Naposimama" aliyoimba na Chid Benz...

Rap Style na Sauti
LANGA Alikua na rap style ya kipekee Sana hakuna msanii hata mmoja aliyekua akifanana naye... Na pia alikua akibadilika kulingana na content ya Ngoma. Mfano Ngoma ya mapenzi kama "Pipi ya kijiti" alirap tofauti na Ngoma ya "Gangster" ambayo inaelezea hustle za kitaa.

Vina na punchline
Jamaa alikua na vina vinavoburudisha alafu n vile vina vya hip-hop na sio Ngonjera mfano kwenye Ngoma ya ni Hayo tu aliyopewa shavu na Fid q aliua Sana namna hii
"Natumia akili, ustarabu na subira..
Situmii nguvu jaziba na hasira..."

Tunammiss Sana Langa, kuna siku nilikua mahabusu... Nilimkumbuka Sana Langa kwenye Ngoma ya Babuu WA kitaa "kimbia" kuna mstari mmoja ulinigusa Sana anasema
"Sio swala la uoga ama kuogopa ukunguru...
Lakini Bora kulogwa kuliko kukosa Uhuru...."

Da chozi lilinitoka sio Kwa sababu nilikua gerezani la hasha! Bali ni Kwa Kua Langa hakua tena duniani...

R.i.p LANGA
 
Umenikumbusha mbali sana

Kuhusu story ya Jaymoe na Langa iko hivi kwenye wimbo aa Jipange wa Jaymoe , Kuna mstari jay moe anasema

" Amani kwa kaka voda milionea/ Wastue wadogo zako waache poda wale mmea/

Hapa alikua akijaribu kumkumbusha Kaka voda awastue kina langa kua Unga sio mzuri

Langa Ni kama alipanic akaja kujibu

Amani kwa kaka voda milionea/ mwambie moe aache ushoga na umbea/

Kupitia hii line Jaymoe alihuzunika sana kwanini anajaribu kuwakumbusha kina langa kuacha matumizi ya unga ila anatukanwa, Haikuishia hapo

Baada ya Langa kuja kustuka kuwa madawa yanamuharibia akaanza kujirudi akatoa project kadhaa na zikafanya vizuri tuu

Mfano Am supplying & Rafiki wa kweli na Kifo jela ah taasisi

Sasa kipindi langa anajitafuta kurudi mainstream baada ya kutoa Am supplying , Kipindi anafanya ngoma ya Rafiki wa kweli ,iliyofanyiwa production na P funk majani,akawa anataka kwenye hii ngoma ya Rafiki wa kweli amshirikishe Jay moe , Lengo ilikua ni kuwaonyesha watu kuwa yeye na Moe hawana matatizo

Alivomtafuta jaymoe ikashindikana coz jaymoe alikua bado ana hasira kwann Langa alimtukana kwenye ile line ya

"Amani kwa kaka voda milionea/ Mwambie moe aache ushoga na umbeya"

Bhas ikabidi langa akomae mwenyewe ngoma nzima ,na ilivotoka ilifanya vizuri sana,

Ikabidi Langa kwenye Ngoma ya Kifo,Jela au taasisi aliweke sawa hilo swala

Kuna line anasema

"Amani kwa kaka voda milionea/ Mwambie Moe sili ngaja wala mmea/

Tukirudi kwa Jay moe, anakiri alivopata habari kuwa Langa amefariki, Alilia sana, na sababu kuu iliyomfanya Moe akalia ni kwamba kipindi Langa yuki hai alijaribu kumtafuta moe mara kadhaa ili wamalize tofauti zao ,ikiwa ni pamoja na kushirikishwa kwenye wimbo wa Rafiki wa kweli ila kiburi chake kikapelekea mpaka Langa anafariki hawaja maliza tofauti zao

Moe anasema hiki kitu kinamuuma sana.


Moja ya line kali nnazozikubali kutoka kwa the late langa ni

Wananichekea usoni kisogoni wananisema/
Wanatafuta mabaya wanajifanya hawaoni mema/

Rest in peace Lyrical And Naturally Gifted African (LANGA)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom