Salamu mzee Lukuvi na wenzako wote wizara ya Ardhi,mimi ninatembelea sana maeneo ya ubungo NHC nyuma ya stendi ya mkoa,Hostel za chuo kikuu cha Dar es salaam na nyuma ya ubungo plaza.
Ni eneo nililoishi kwa miaka mingi kabla ya kuhama miaka mitatu iliyopita,eneo hilo lilikuwa na nyumba ndogondogo maarufu kwa jina la Kota,nyumba hizo zilijuwa zikimilikiwa na shirika la nyumba la taifa(NHC)kabla ya kuziuza kwa wapangaji wake miaka kadhaa iliyopita.
Eneo lilikuwa limepimwa,lakini kero iliyopo ni kuwa;pamoja na upimaji ambao uliacha barabara pana sana na kufanya mandhari nzuri lakini sasa barabara za ebeo hilo zimebanwa sana kutokana na watu kuongeza maeneo yao pamoja na kuweka vibanda vya biashara kiasi kwamba linaonekana kama"squarter".
Juzi tu gari zimekwaruzana na kusabaisha foleni kali sana,na nilisikia ni kero ya muda mrefu sana hali hiyo inapotokea.
Nakuomba mheshimiwa pita huko muwakumbushe wananchi mipaka