Lukuvi atangaza kiama

News TZ

Senior Member
Jun 17, 2015
127
69
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi amesema hatasita kuwafukuza kazi baadhi ya watumishi wa wizara hiyo ambao watabainika kujihusisha na vitendo vya wizi, udanganyifu katika ugawaji ardhi na viwanja kwenye halmashauri. Amesema anaamini hatua hiyo itasaidia kukomesha tabia mbaya iliyojengeka miongoni mwa watumishi wa idara ya ardhi katika maeneo mbalimbali ya hapa nchini ambao huwatapeli wananchi kwa lengo la kujinufaisha kibinafsi.

Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akisikiliza kero za wananchi katika ziara yake katika wilaya za Tanga na Muheza mkoani Tanga.\ “Mwaka huu wa 2016 serikali imejiwekea lengo kwamba ndio uwe mwaka wa mwisho wa kumaliza migogoro ya ardhi iliyokuwepo tangu uongozi wa awamu ya kwanza, ya pili, ya tatu na ya nne ndiyo maana wizara ya ardhi tumelazimika kuweka wazi suala hilo na mikakati ya kukabiliana nayo”, alisema.

Waziri huyo alisema kwa sababu ya kukithiri kwa vitendo hivyo vya ukiukwaji wa sheria unaofanywa na baadhi ya watendaji wasio waaminifu kuvunja sheria kwa makusudi kwa kutegemea kuonywa au kuhamishwa kituo cha kazi, wizara imeamua kuchukua hatua.

“Watumishi waliofanya makosa baada ya tume au kamati za kutatua migogoro katika eneo husika zitakapowabaini, wizara yangu itachukua hatua za haraka kwanza kwa kuwasimamisha kazi wakati wa uchunguzi na itakapothibitika watafukuzwa mara moja”, alisema.

Aidha alisema, “Hatuwezi kuendelea kuruhusu uwepo wa watumishi kama hawa kwa sababu mwananchi anapolipa fedha zake kupatiwa kiwanja lakini unakuta lengo la mwananchi halifikiwi na badala yake anaingizwa mkenge kwa kujikuta wamegawia watu watatu kiwanja kimoja”.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza, katika taarifa yake kuhusu migogoro, alimweleza waziri huyo kwamba mkoa wa Tanga una migogoro mingi ya ardhi na imetokana na baadhi ya watumishi wa mabaraza ya kata na wilaya kutoheshimu hati za kimila.

Alisema idadi kubwa ya wananchi wanaopelekwa katika mabaraza hayo wakiwa na hatimiliki za kimila kwa kiasi kikubwa wamedai hawapewi ushirikiano na kwamba viwango vya fidia wanavyolipwa havina uhalisia. “Fidia ilishatolewa muongozo na serikali tangu mwaka 2013 na viwango dira vya malipo vikawekwa lakini wanavyolipwa kwa sasa wananchi wetu vya fidia havilingani kabisa na uhalisia wa mali zao,” alisema. Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliotoa malalamiko yao kwa Lukuvi walionesha kutokuwa na imani na watendaji wa halmashauri kitengo cha ardhi na kumuomba waziri kuingilia kati ili wapate haki zao kwa haraka.

Chanzo: darwaya.com
 
asianzishe sinema mpya,ye bora afanye kaz2,..hayo tumesikia sana kwakweli bt mwisho wa siku ni yaleyale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…