Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 46,626
- 66,816
Luhaga Mpina umekuwa machachari sana kuiwajibisha serikali ya chama chako tofauti na wabunge wenzako wengine wote wa chama chako. Kama utaendelea na mwendo huo unaweza kuleta mabadiliko makubwa mno ukiwa ndani ya CCM kuliko nje yake.
Wewe sasa hivi unachukuliwa kama nembo ya ujasiri ndani ya chama chako kama vile alivyokuwa Benard Membe. Tofauti na wakati wa Membe sasa mazingira ya kufanya siasa yameboreka kiasi na ndio maana mpaka sasa hujaitwa na kamati ya maadili na hakuna dalili za kukufukuza kutoka ndani ya chama au kuundiwa zengwe lolote.
Usizifuate njia za Lowassa, Slaa, Nyalandu na Membe za kuhama chama, wananchi wengi wamezichoka siasa za aina hiyo, utawapoteza kujitoa katika chama chako.