the guardian 17

Senior Member
Aug 15, 2024
199
311
Ni ukweli usiopingika kuwa miongoni mwa nyenzo muhimu katika kujifunza maarifa fulani ni lugha, lugha ndiyo hutumika kuhifadhi maarifa mbalimbali lakini pia ndiyo njia ya mawasiliano. Kila taifa lina lugha zake maaulumu za kufundishia kutokana na sababu mbalimbali walizojiwekea wao kama nchi.

Nchini Tanzania Lugha za kufundishia kwa mujibu wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 inaeleza kuwa Lugha ya kufundishia ni kiswahili na kiingereza, ambapo zimegawanyika kama ifuatavyo

Elimu ya awali na msingi

Lugha ya kiswahili inatumika katika kufundishia elimu ya awali na msingi na hufundishwa kama somo, wakati kiingereza inatumika kama lugha ya kufundishia katika baadhi ya shule za msingi kwa utaratibu maalumu.

Elimu ya sekondari, vyuo vya ualimu (diploma) na vyuo vya elimu ya juu

Pia lugha ya kiingereza inatumika kama lugha ya kufundishia katika shule za sekondari , vyuo vya ualimu ngazi ya stashahada, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya juu wakati kiswahili kikifundishwa kama somo.

Ualimu ngazi ya cheti na vyuo vya ufundi stadi

Kiswahili kinatumika pia kama lugha ya kufundishia katika vyuo vya ualimu ngazi ya cheti, vyuo vya ufundi stadi na baadhi ya shule za sekondari inapohitajika.

Masomo ya kujenga na kuendeleza maadili

Masomo haya yatatumia lugha ya kiswahili katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

Mjadala kuhusu lugha ya kufundishia

Mijadala mbalimbali imeendelea kuwepo kuhusu ni ipi iwe lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Wadau mbalimbali wamekuwa wakiwa na maoni tofautitofauti ambapo wengine wamekuwa wakipendekeza lugha ya kufundishia iwe ya kiswahili kwa ngazi zote kuanzia awali kwa shule za serikali hadi vyuo vikuu kwani itapunguza baadhi ya changamoto ikiwemo kufeli kwa wanafunzi hususani kuanzia ngazi ya sekondari kutokana na mchanganyiko wa lugha za kufundishia.



Screenshot 2025-01-23 075134.png


Baadhi ya mijadala
Soma: Serikali inaogopa nini kufanya lugha ya kufundishia iwe kingereza kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu?

Soma: Kwani serikali ya Tanzania inalazimisha lugha ya kufundishia elimu ya awali na msingi iwe Kiswahili

Soma: SoC04 - Lugha ya kufundishia na kujifunzia katika mfumo wa Elimu Tanzania
 
Back
Top Bottom