singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
CCM ni chama kongwe hakiishiwi mbinu, na mbinu kubwa ya katika uchaguzi mkuu uliopita na kumwingiza ikulu Tingatinga Dk Magufuli ilikuwa ni kumzuia Lowassa kwa njia ya chukizo kubwa ili alazimishwe kuondoka na kuhamia upinzani, kwa maana ya Ukawa.
Ukawa bila kujua walimpokea Lowassa kwa mikono yote miwili, na kwa CCM Lowassa kuhamia Chadema ilikuwa na kugombea Urais ilikuwa ni sawa na jiwe moja kuua ndege wanne kwa maana Cuf, Chadema, Nccr Mageuzi na NLD, Jiwe moja tu linaloitwa Dk. Magufuli likaisamabaratisha ukawa chali kabisa.Kwa hiyo kama kuna Mwanasiasa anaamini kuwa ccm imetumia nguvu nyingi katika kumkabili Lowassa katika uchaguzi wa mwaka huu basi huyo hajui kusoma alama za nyakati.
Ukweli ni kwamba kutokana na hali ya mwamko ulivyokuwa na wananchi kuchoka kutokana na ufisadi mbalimbali ukiwemo wa Richmond ESCROW nk walikuwa wapo radhi kujaribu chama kingine badala ya ccm walikuwa wako tayari hata kuchagua jiwe au hata shetani kama ccm ingemsimamisha mgombea mwingine zaidi ya Dk. Magufuli.
Lowasa alikuwa ni chambo katika uchaguzi huu, chambo amabcho kilimezwa na chdema, hivyo kuihakikishia ccm kuendelea kushika hatamu za uongozi nchi hii.
Sumaye na mzee Kingunge walikuwa hawakumuelewa kabisa mwenyekiti wa ccm, rais mstaafu Jakaya kikwete katika maonyo yake ya kila siku akiwataka ccm wasibwetete kwani ccm inaweza kungolewa madarakani hivyo wajiandae kisaikolojia kauli hiyo iliwafanya hata Ukawqa nao kubweta huku wakifurhi front page za magazeti ambayo yalikuwa bize kufanya biashara.
Lakini baada ya Chadema kunasa chambo cha kwanza na kuongezeka chambo wengine Sumaye na Kingunge wakidhani kuwa ndiyo tiketi ya kwenda ukawa, ndipo hapo sasa JK , Mangula walipoanza kuliandaa Tingatinga vilivyo na ilkikuwa nusuru JK awangamue ukawa pale aliposeama ccm tuna mbinu lakini ukawa walibaki usingizini tena usingizi wa pono
Wakati Nape akitumika kuwahadaa na bao la mkono ambalo lilihamisha fikra za kina Mbatia,lissu na Mbowe pamoja na Kinaa Mnyika ambao walikuwa wakitumia muda mwingi kujihami pasipo kushambulia Jk aliweka wazi kwa kusema cc mina mbinu lakini ukawa walikuwa wakifurahi chmbo walichotegewa wakiota ndoto za ikulu mchana wa saa nane. Waliingia katika mtego wa chambo na wakahadaika kweli na chambo hicho.
Wakongwe wa siasa nchini Rais Mstaafu wa awamu ya pili mzee ruska akawachanganya kabisa alipowaambia wananchi wasichague ccm b wakati ccm a ipo. Mzee mkapa akawamaliza kabisa kwa kuwaita malofa waliofirisika.
Ukawa kwa kuitwa malofa kuliwafanya wachanganyikiwe kabisa na kuanza kulalama wakiomba huruma ya wapiga kura haliyakuwa wapiga kura wao walikuwa bize kusikiliza sera na wao hawakuwa na sera hivyo wapiga kura wakawa wanamsikiliza zaidi magufuli baada ya chambo kushindwa kabisa kusema atawafanyia nini akiwahimiza zaidi kwenda kusoma website wakati watanzania na wapiga kura wengi wa vijijini hawajui hata maana ya website wananchi na yeye akiwa hamalizi hata dakika tano jukwaani.
Mwisho kabisa nimalizie kwa kusema Uamuzi wa Lowasa kuondoka kwa hasira ndani ya ccm kasha kufatwa na kina Sumaye na Kingunge na baada kufika huko wakIteka mamlaka na nguvu zote ndani ya Ukawa ndiyo umeikoa CCM na kuisalimisha Kuifuata KANU ya Kenya n UNIP ya dk. Kaunda.
Naamini kwa serikali ya sasa ya Dk Magufuli ambayo imeonyesha kukubalika kwa asilimia 90 na watanzania itafanya mabadilko makubwa serikali na ndani ya chama mabadiliko amabayo yatakuwa na tija kubwakwa watanzania hivyo basi itachukua takribani miaka 20 au 30 kwa Tanzania kushuhudia uchaguzi uliokuwa na vutanikuvute kama wa mwaka huu,
Na katika hilo mabadilko ndani ya chama hata pata kazi kubwa baada ya magamba yote kujivua kiulani na yaliyobaki hayana nguvu na siku zao zinahesabika na Kinana keshaanza kuyamwagia mafuta ya taa kabla kuyatia kiberiti,wakati JK na Mangula wanachofanyai ni kuhakikisha anamrahisishia kazi magufuli ndani ya chama ili aikute ccm yenye umoja na nidhamu kwa kuwa watakuwa wameshaumaliza mtandao wote ulikuwa na jeuri ya fedha ndsani ya chama hicho.