Lowassa ataja sababu ya TB Joshua kutohudhuria sherehe za kuapishwa Rais Magufuli

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,489
Aliyekuwa mgombea urais
kwa tiketi ya Chadema,
Edward Lowassa, jana
aliweka wazi jinsi alivyoweza
kumshawishi Muhubiri
maarufu kutoka nchini
Nigeria, T.B Joshua
kutohudhuria sherehe za
kuapishwa kwa Rais John
Magufuli, ingawa aliletwa
nchini na CCM.

Akizungumza jana katika
mahafali ya Shirikisho la
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu
Wafuasi wa Chadema
(Chaso), Lowassa ambaye
alieleza kuwa ni rafiki wa
karibu wa T.B Joshua wa
Synagogue Church Of All
Nations (SCOAN), alisema
kuwa CCM ndio waliomualika
mhubiri huyo kuja nchini kwa
lengo la kuhudhuria sherehe
za kuapishwa kwa Rais
Magufuli na kumshawishi
[Lowassa] akubaliane na
matokeo ya uchaguzi huo.

“Walimuita rafiki yangu TB
Joshua, wakaenda
wakampokea. Alipokelewa na
Rais Magufuli, akapelekwa
Ikulu akazungumza na
Kikwete. Baadaye
akawaambia wamlete
kwangu. Kweli akaja
nyumbani kwangu,
tukazungumza naye. Sitaki
kusema mengi sana
niliyomwambia, lakini moja,
nilimwambia ukikubali yale
matokeo ndugu yangu,
heshima yako itashuka hapa
nchini na duniani kwa
ujumla,” Lowassa
anakaririwa.

Lowassa alieleza kuwa yeye
pamoja na viongozi wengine
wa Ukawa walikutana na T.B
Joshua na kumueleza kuhusu
uchaguzi ulivyoendeshwa na
alikubaliana nao. Kutokana
na kukasilishwa na maelezo
hayo, Mhubiri huyo alibadili
utaratibu
aliokuwa ameandaliwa na
wenyeji wake na kuendelea
na utaratibu wake kabla
hajaondoka nchini bila
kuhudhuria tukio hilo la
kihistoria (Novemba 4, 2015).

Mwanasiasa huyo mkongwe
alielendelea kusisitiza kuwa
alishinda uchaguzi uliopita
lakini ushindi wake uliporwa
na CCM.
“Tulishinda vizuri sana lakini
hata hizo walizotupa,
zinatosha kuwaambia kuwa
tuliwapa kazi ya kutosha.
Nyie mnajua, wao wanajua
na mimi najua,” alisema.

T.B Joshua aliingia nchini
Novemba 3 mwaka jana na
kupokelewa na Rais John
Magufuli katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere na kisha kuelekea
Ikulu ambapo akikutana pia
na Rais Mstaafu, Jakaya
Kikwete na viongozi wengine.
Baadae, Mhubiri huyo
alionekana akiwa na viongozi
wa Ukawa nyumbani kwa
Lowassa na kufanya ibada
maalum siku iliyofuata kabla
ya kuondoka nchini, matukio
ambayo yaliacha maswali
mengi kwa wafuatiliaji.

Mwaka 2011, Rais Magufuli
akiwa Waziri wa Ujenzi,
alienda Nigeria na kuhudhuria
idaba katika kanisa la T.B
Joshua na baadae yeye na
familia yake walikutana na
Mhubiri huyo na kupiga picha
kadhaa zilizoonekana kwenye
mitandao ya kijamii. Mwaka
2012, Lowassa pia
alihudhuria ibada katika
kanisa hilo akwia na mkewe
na walifanya hivyo mara
kadhaa. Mwingine aliyewahi
kuhudhuria ibada katika
kanisa hilo ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba na hivi
karibuni, Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe
alionekana katika kanisa hilo.
 
Kumbe mwepesi kama kumdanganyia mtoto mdogo peremende?!!
 
Aliyekuwa mgombea urais
kwa tiketi ya Chadema,
Edward Lowassa, jana
aliweka wazi jinsi alivyoweza
kumshawishi Muhubiri
maarufu kutoka nchini
Nigeria, T.B Joshua
kutohudhuria sherehe za
kuapishwa kwa Rais John
Magufuli, ingawa aliletwa
nchini na CCM.

Lowasa hamjui TB JOSHUA.
Katika vitu ambavyo ni mwiko kwa TB JOSHUA ni kuhudhuria sherehe ya aina yoyote nje ya zile za Kanisa lake.
Hata kwao Nigeria hahudhurii sherehe iwayo yoyote.
Ameshapewa nishani kibao na serikali ya Nigeria lakini hata siku moja huwa hataki kuhudhuria sherehe hizo za kupewa hizo nishani kwa kusema kuwa hapendi utukufu wa kidunia.Angetaka angeweza hata kuwa mgeni wa heshima wa sherehe za nchi kibao ila huwa hataki kabisa na haendi.

Muulize Lowasa toka TB joshua aanze huduma yake aliwahi hudhuria sherehe wapi?

LOWASA ufahamu wake mdogo na hana washauri wala wachambuzi wa mambo wa kumsaidia.
 
Bavicha ni wepesi sana kuchotwa! CCM waliona mbali kweli kama mzazi anayempa mtoto ice cream ili anyamaze ila ikiisha ndo anakuja kugundua baadae sana.
 
Katiba ya kanisa lake ndivyo inavosema au ni uamuz tu akibadiri anakwambia au !!?
 
Kwan ile ilikuwa ni sherehe?
 
Hii itakuwa ni kweli 100% coz CCM hao ndio walituhaminisha kuwa Joshua kaja kushuhudia magu akiapishwa. Na magu ndye alimpokea.
 
Wadau ebu nisaidieni EL anasema hatambui matokeo lkn kila anapotamka jina la Magufuli lazima
aanze na neno RAIS
 
Kuchanganyikiwa kumeanza,mbona tumeshasahau mambo ya uchaguzi na kuapishana
 
Amekosa jambo la kuongea.TB Joshua ni nani nchi hii? Ivi kumbe Lowasa anamwabudu TB
 
wakurya sio wajinga wanawake kuoa waliona mbali ifikie hatua tuache kung'ang'ania kuajili mabaunsa na mabodigadi kutulinda umri ukishaenda sana akili zinakuwa za kitoto hata kuwaza tunawaza kama watoto wadogo ifikie hatua tuajili washauli watusaidie baadhi ya mambo.
 

Sawa msemaji wa TB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…