Zimetupwa wapi njia zile zilizokuwa zikitumika kupata mke bora...Njia zile zilizotupa fursa kujua hadi kwenye shina la familia la umpendae kabla hata ya kutangaza uchumba, Njia zile zilizokuwa zinakupa hadi uhakika wa tabia ama asili ya familia ya umpendaye kuanzia mababu zao, mila na matambiko yao, magonjwa, laana katika familia yao...Hakika technologia imekuja na changamoto zake nyingi sana...Unatafuta mke kwenye mitandao hujui hatakuwa jini ama mzimu hata wapi katoka hujui halafu unakuta watu wamekaa kwenye vijiwe wanasema hivi mbona ndoa za siku hizi hazizidumu kama zamani...20% wanabahatisha wake/waume zao ila 80% ya staili hizi za wachumba wa mitandaoni wanaangukia pua...