Loliondo Facts Check: Mshindani wako anapojigeuza mshauri mwema

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
765
939
MSHINDANI WAKO ANAPOJIGEUZA MSHAURI MWEMA. LOLIONDO FACTS CHECK

SIKU Ukiona Mshindani wako katika jambo mnalishindania anakusauri juu ya kufanikiwa kwako kwenye jambo hilo JITAFAKARI SANA

Ushauri wake kweli utakuwezesha kumshinda na kulifukia lengo lako?.

Namaanisha HIVII, Siku Yanga ikaishauri Simba namna Bora ya kusajili wachezaji, na SIMBA ikasajili Kwa maelekezo ya Yanga, itakachokutana nacho ni simulizi za Karne

KAMWE, KAMWE, KAMWE SIO RAHISI

Hivi si mnakumbuka washindani wetu waliitangazia Dunia kuwa mlima Kilimanjaro upo kwao?. Na Dunia ikabaki chembe tu iamini hadi tulipoionyesha ukweli

Lakini hata Dunia ilipotambua kuwa Mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania, unafikiri wameacha kujitapa nao?.

Sasa hivi wanasema ukitaka kuuona mlima Kilimanjaro njoo kwetu, yaani kwaooo.


Nasema HIVII, si mnakumbuka mbwana samatta alivyosajiliwa ULAYA?....walisemaje vileee, walisema ni wa kwao

Wenzetu hawa linapokuja suala la maslahi ya kwao na nchi yao Wala hawana Soni usoni Wala mioyoni.

NIWAKUMBUSHE KITU?.

Mmesahau eeeee?. Si mnakumbuka siku ROYAL TOUR inakaribia kuzinduliwa?.

Wakamtengeneza binti mnaijeria na kuporomosha tuhuma lukuki kuhusu Zanzibar, Tufanye Tuhuma zoooote zilikuwa kweli, je kwanini sasa waliziporomosha wakati wa Royal Tour?....Jibu unalo

Leo Serikali ya TANZANIA imeamua kuwagawia wananchi wake wa Loliondo kilomita za mraba 2500 na kuzihifadhi 1500 kwa maslahi ya Taifa pamoja na hifadhi zao, wanatoka barabarani bila aibu wanajidai wamepigwa, Eti watoto wao wamepigwa?.... Wanamshauri Rais Samia azuie zoezi la kunusuru Hifadhi zetu kuwa malisho wa Mifugo yao kama ealivyozoea.

Ndugu zangu tuendelee kuwa macho.

Hakuna Mshindani anayemtakia mema Mshindani wake.
 

Attachments

  • VID-20220613-WA0213.mp4
    11.2 MB
Back
Top Bottom