"Little Bastard":Gari iliyolaaniwa katika Uso wa Dunia

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,274
6,592
c75b39d583a790a6cdce6d7c181cf01fab0477d4_hq.jpg

IJUE GAR YA MR JAMES ILIYO LAANIWA DUNIANI
1332268489_55c9f504b5_o.jpg

Katika dunia kuna mambo mengi sana ya kushangaa ambayo kwa namna moja au nyingine huweza kuamini kuwa mambo haya yalipangwa kwa namna moja ama nyingine.

Tumeona historia ya mrais wawili wa marekani walioshi maisha yaliyofanana kwa asilimia kubwa katika uzi huu Nani aliyepanga haya mauaji ya hawa Marais Abraham Lincoln na John Kennedy? .Katika matukio haya tunaona kuwa uhalisia wa maisha ya duniani haupo kama tunavyouona .Hakika dunia ina mengi sana ya siri ambayo kwa ulimwengu huu wa kawaida hatuwei kuona chochote zaidi ya kushabikia tu pasipo evidence na kuita uchawi au ushirikia kama wengine wanavyosema.

Ila tukubali tukatae kuwa ulimwengu huu unavingi sana ambavyo havijafunuliwa kwa macho ya kawaida.

Ni wengi sana humu JF wamekuwa mashahidi wa namna watu wanavyotumia nguvu kubwa kusema kuwa ni uchawi,ulimwengu uliofichwa unapofunuliwa kwa kiasi kidogo hugeuzwa ni SIASA na story za kufurahisha na kupetezea muda zaidi ya kukubali ukweli kuwa hapa duniani haujui vingi sana. Matukio kama haya yanaweza kuwa chachu kwa mpenda kufahamu mambo mbali mbali mengi yasiyoonekana kwa macho ya kawaida yenye nguvu kubwa sana kwa ulimwengu wa sasa. Ni wangapi humu JF waliweza kufungua thread hii Mambo 6 Duniani yaliyotokea kwa namna ya kuacha Mdomo wazi

Sasa imefika hatua inabidi tukubali kuwa ulimwengu haupo kama unavyoufikiria wewe.

Mkuu mshana alijitahidi kutuelesha kuhusu picha katika thread hii Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho shaka hakuna mtu aliyetoka bila kukubaliana na mshana katika hii thread baada ya kujaa evidences zenye kila sifa ya kukushawishi kuwa ulimwengu huu ni zaidi ya unavyoufahamu.

SASA TURUDI KWENYE MADA HUSIKA

Wengi humu JF linapokuja jina la James Dean huchukulia ni jina kama majina mengine hivyo huona hakuna kitu cha kushtusha katika jina hilo.Ila ni wachache sana wanaweza kushtuka kuona kwanini Jina La James Dean limekuwa likijirudia mara kwa mara masikioni mwake?

Story inaanzia hapa:
James+Deans+car+curse.png



James Dean alikuwa na gari yake nzuri sana ambayo aliita "Porsche",ni gari ambayo mda mfupi baadae ikachukua maisha yake.Ni gari ambayo ililaaniwa duniani.

James Dean alikuwa na gari yake ya mashindano hivyo akaibadilisha aina ya gari yake kutoka 356 kuwa 550 Spyder porsche.James dean akalilemba gari yake hii mpya kwa kubadili rangi ya viti ndani ya gari kuwa rangi nyekundu.
421_p5_l.jpg



Hakika maswali ni mengi sana kuliko majibu,kuna mengi zaidi ya kushangaza kuhusu gari hili.

Gari hili lenye laana halikumuua James tu bali lilimuua kila mtu aliyejaribu kulitumia kwa namna yoyote ile.

Baada ya kikao cha muda mrefu cha wanafamilia wa James Dean hatimaye wakakubalina kuuza gari hilo kwa George Barris(ambaye ndio aliyelitengenea gari hilo ) kwa dollar 2500.

Kama ilivyo kwa wafanya biashara na hatimaye akaamua kuchoma "Baadhi ya vifaa " kutoka kwenye gari iliyoharibika na kuviuza.Siku ya mnada walitokea watu wengi sana kwenda kununua hasa engine.

Barris alifanikiwa kuuza baadhi ya vifaa vya gari kwa madereva wawili wa mbio za magari,engine kwa Troy McHenry na drivetrain kwa William Eschrid.
hqdefault.jpg


Bwana Troy na William wakiwa katika mashindano ya mbio za magari wakitumia magari yaliyowekwa vifaa walivyovinunua kutoka kwa Barris ,Troy McHenry akapoteza uelekeo na kugonga mti na alikufa hapo hapo huku Mr William alipata majeraha makubwa sana baada ya gari yake kupinduka zaidi ya mara mbili.

Huku kwa Mr Barris alikuwa amebakiwa na matairi mawili kutoka kwenye gari ya James ambayo hakuyauza na hivyo akaamua na kupelekea mnunuzi muda mfupi baadae kupata ajari mbaya baada ya matairi hayo kuchomoka akiwa barabarani.Alikufa hapo hapo!
James-Dean-Car-Curse.jpg


Bwana Barris akaamua kuliweka gari bila kuuza baadhi ya vifaa.Vijana wawili wezi walivutiwa sana na matairi mengine yaliyobaki na siti za gari hivyo wakakubaliana kuwa wasogee taratibu wakaibe vifaa hivyo.Mmoja akasogea kwenye tairi la gari ambapo alipokuwa anajaribu kufungua tairi mkono wake ukachanika na kipande cha chuma kilichokuwa kinaning'inia pembeni ya rim ya tairi la gari.Mwizi mwingine ambaye alikuwa anajaribu kufungua siti za gari akajikuta akibanwa na vyuma na kupelekea kushindwa kutoka.
james-dean-397027_640-600x400.jpg

(James Dean)
Kutokana na mikasa yote hii iliyokuwa inaikumba gari hatimaye Barris akaamua kulifungia jumla gari lake ndani ila wazo hilo lilipingwa na " California Highway Patrol" ambao walimwambia gari hili inabidi liende garage kwa matengenezo zaidi.

Baada ya gari kufika garage ilikaa siku moja na siku ya pili garage hiyo iliwaka moto ambao haukuligusa gari hata kidogo.Gari lilibaki salama kabisa!

California Highway Patrol wakaamua sasa gari lisafirishwe kwenda sehemu nyingine kwa matengenezo zaidi.

Laana iliendelea baada ya gari lililolibeba kupata ajari njiani ambapo dereva wa gari alipoteza uelekeo na kupelekea dereva kurushwa nje na kugongwa na gari iliyokuwa inakuja nyuma yake na kufariki papo hapo.

Gari iyobebwa ikarushwa na kuangukia magari mengine mawili ambapo haikumdhuru yeyote aliye ndani ya gari.



5468ac23f4d7557c6e98b3926ce0bbe8.jpg



HUU NDIO ULIMWENGU TUNAOISHI
article-2303428-003641A200000258-193_638x416.jpg


SENGWILE MAKAMANDA
Deadbody
 
Internet imejaa mambo mengi unapaswa kutumia akili kujua ipi pumba upi mchele, wewe umechagua pumba tupu. Obi-Wan kenobi na sio Obi-Wan Kebobi, pia Obi sio mtu halisi bali na character kwenye movies za "Star Wars" kama umewai kuziona, Katika movie hizo Obi-Wan Kenobi (nafasi iliyoigizwa na sir Alec Guiness) ni "Jedi", kwenye hiyo movie baada ya sayari moja kuangamizwa na siraha mpya iliyoitwa "death star" Obi kwa kutumia "force" aliweza kuhisi msiba huo akiwa kwenye sayari nyingine kabisa.

Sasa je habari ya James Dean na Obi inatoka wapi? Sir Alec (aliyeigiza kama Obi) akiwa kwenye interview mwaka 1977 aliulizwa kama amewahi kuhisi hiyo paranornal experience (kupata hisia fulani mtu unaye mfahamu akifa japo unakua bado hauna taarifa) kwenye maisha halisi, akajibu ndio, ilimtokea James Dean alipokufa kwenye ajari.

Pia je ni kitu gani kinaifanya ajari ya Dean kuwa kitu cha kuongelea? Wakati dean anakufa alikua na miaka 24 tu, taarifa za kiusalama zinadai alikua akiendesha kwa speed kali tena hovyo lakini mtu pekee aliyeshuhudia ajari hiyo ambae bado yuko hai anadai Dean hakua akiendesha siku hiyo bali ni Fundi magari wake ndio alikua nyuma ya usukani.
 
KUTOKANA NA USUMBUFU KUWEKA UZI JUKWAA LA INTELLIGENCE NIMEAMUA KUWEKA HUKU NA MODS WATAHAMISHA KULE.

c75b39d583a790a6cdce6d7c181cf01fab0477d4_hq.jpg

IJUE GAR YA MR JAMES ILIYO LAANIWA DUNIANI
1332268489_55c9f504b5_o.jpg

Katika dunia kuna mambo mengi sana ya kushangaa ambayo kwa namna moja au nyingine huweza kuamini kuwa mambo haya yalipangwa kwa namna moja ama nyingine.

Tumeona historia ya mrais wawili wa marekani walioshi maisha yaliyofanana kwa asilimia kubwa katika uzi huu Nani aliyepanga haya mauaji ya hawa Marais Abraham Lincoln na John Kennedy? .Katika matukio haya tunaona kuwa uhalisia wa maisha ya duniani haupo kama tunavyouona .Hakika dunia ina mengi sana ya siri ambayo kwa ulimwengu huu wa kawaida hatuwei kuona chochote zaidi ya kushabikia tu pasipo evidence na kuita uchawi au ushirikia kama wengine wanavyosema.

Ila tukubali tukatae kuwa ulimwengu huu unavingi sana ambavyo havijafunuliwa kwa macho ya kawaida.

Ni wengi sana humu JF wamekuwa mashahidi wa namna watu wanavyotumia nguvu kubwa kusema kuwa ni uchawi,ulimwengu uliofichwa unapofunuliwa kwa kiasi kidogo hugeuzwa ni SIASA na story za kufurahisha na kupetezea muda zaidi ya kukubali ukweli kuwa hapa duniani haujui vingi sana. Matukio kama haya yanaweza kuwa chachu kwa mpenda kufahamu mambo mbali mbali mengi yasiyoonekana kwa macho ya kawaida yenye nguvu kubwa sana kwa ulimwengu wa sasa. Ni wangapi humu JF waliweza kufungua thread hii Mambo 6 Duniani yaliyotokea kwa namna ya kuacha Mdomo wazi

Sasa imefika hatua inabidi tukubali kuwa ulimwengu haupo kama unavyoufikiria wewe.

Mkuu mshana alijitahidi kutuelesha kuhusu picha katika thread hii Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho shaka hakuna mtu aliyetoka bila kukubaliana na mshana katika hii thread baada ya kujaa evidences zenye kila sifa ya kukushawishi kuwa ulimwengu huu ni zaidi ya unavyoufahamu.

SASA TURUDI KWENYE MADA HUSIKA

Wengi humu JF linapokuja jina la James Dean huchukulia ni jina kama majina mengine hivyo huona hakuna kitu cha kushtusha katika jina hilo.Ila ni wachache sana wanaweza kushtuka kuona kwanini Jina La James Dean limekuwa likijirudia mara kwa mara masikioni mwake?

Story inaanzia hapa:
James+Deans+car+curse.png



James Dean alikuwa na gari yake nzuri sana ambayo aliita "Porsche",ni gari ambayo mda mfupi baadae ikachukua maisha yake.Ni gari ambayo ililaaniwa duniani.

James Dean alikuwa na gari yake ya mashindano hivyo akaibadilisha aina ya gari yake kutoka 356 kuwa 550 Spyder porsche.James dean akalilemba gari yake hii mpya kwa kubadili rangi ya viti ndani ya gari kuwa rangi nyekundu.
421_p5_l.jpg

Dean baada ya kulinunua gari hilo akamfuata rafiki yake na kumpa habari ya gari yake mpya aliyoinunua.Obi-Wan Kebobi alikubali kuongozana na Dean kwenda kuliona gari lake mpya aliyoinunua namna ilivyo imara na mara gafla akamwambia "Kama ukitumia gari hili nauhakika litakuua ndani ya siku 7 tu hivyo achana nao".Ni jambo gumu sana kukubalina na wazo kama hili kwa kitu chako kipya cha thamani kubwa ulichonunua muda sio mrefu hivyo Mr James Dean akaamua kuendelea kulitumia gari lake hili mpaka week ijapo alikufa akiwa ndani ya gari hilo.Hapa tunasema utabiri wa Mr Obi-Wan Kebobi umetimia hivyo Mr james Dean aliuliwa na gari yake mwenyewe aliyoinunua kwa thamani kubwa zaidi kuliko vitu alivyovinunua before..

Kwanini Obi-Wan Kebobi alisema vile? Ni fumbo ambalo hata yeye alipokuja kuojiwa baada ya kifo cha James alisema "SIJUI " kwanini nilisema vile maana haikuwa akili yangu iliyoamua kusema vile.Je kuna nini kilijificha nyuma ya pazia??

Hakika maswali ni mengi sana kuliko majibu,kuna mengi zaidi ya kushangaza kuhusu gari hili.

Gari hili lenye laana halikumuua James tu bali lilimuua kila mtu aliyejaribu kulitumia kwa namna yoyote ile.

Baada ya kikao cha muda mrefu cha wanafamilia wa James Dean hatimaye wakakubalina kuuza gari hilo kwa George Barris(ambaye ndio aliyelitengenea gari hilo ) kwa dollar 2500.

Kama ilivyo kwa wafanya biashara na hatimaye akaamua kuchoma "Baadhi ya vifaa " kutoka kwenye gari iliyoharibika na kuviuza.Siku ya mnada walitokea watu wengi sana kwenda kununua hasa engine.

Barris alifanikiwa kuuza baadhi ya vifaa vya gari kwa madereva wawili wa mbio za magari,engine kwa Troy McHenry na drivetrain kwa William Eschrid.
hqdefault.jpg


Bwana Troy na William wakiwa katika mashindano ya mbio za magari wakitumia magari yaliyowekwa vifaa walivyovinunua kutoka kwa Barris ,Troy McHenry akapoteza uelekeo na kugonga mti na alikufa hapo hapo huku Mr William alipata majeraha makubwa sana baada ya gari yake kupinduka zaidi ya mara mbili.

Huku kwa Mr Barris alikuwa amebakiwa na matairi mawili kutoka kwenye gari ya James ambayo hakuyauza na hivyo akaamua na kupelekea mnunuzi muda mfupi baadae kupata ajari mbaya baada ya matairi hayo kuchomoka akiwa barabarani.Alikufa hapo hapo!
James-Dean-Car-Curse.jpg


Bwana Barris akaamua kuliweka gari bila kuuza baadhi ya vifaa.Vijana wawili wezi walivutiwa sana na matairi mengine yaliyobaki na siti za gari hivyo wakakubaliana kuwa wasogee taratibu wakaibe vifaa hivyo.Mmoja akasogea kwenye tairi la gari ambapo alipokuwa anajaribu kufungua tairi mkono wake ukachanika na kipande cha chuma kilichokuwa kinaning'inia pembeni ya rim ya tairi la gari.Mwizi mwingine ambaye alikuwa anajaribu kufungua siti za gari akajikuta akibanwa na vyuma na kupelekea kushindwa kutoka.
james-dean-397027_640-600x400.jpg

(James Dean)
Kutokana na mikasa yote hii iliyokuwa inaikumba gari hatimaye Barris akaamua kulifungia jumla gari lake ndani ila wazo hilo lilipingwa na " California Highway Patrol" ambao walimwambia gari hili inabidi liende garage kwa matengenezo zaidi.

Baada ya gari kufika garage ilikaa siku moja na siku ya pili garage hiyo iliwaka moto ambao haukuligusa gari hata kidogo.Gari lilibaki salama kabisa!

California Highway Patrol wakaamua sasa gari lisafirishwe kwenda sehemu nyingine kwa matengenezo zaidi.

Laana iliendelea baada ya gari lililolibeba kupata ajari njiani ambapo dereva wa gari alipoteza uelekeo na kupelekea dereva kurushwa nje na kugongwa na gari iliyokuwa inakuja nyuma yake na kufariki papo hapo.

Gari iyobebwa ikarushwa na kuangukia magari mengine mawili ambapo haikumdhuru yeyote aliye ndani ya gari.



5468ac23f4d7557c6e98b3926ce0bbe8.jpg



HUU NDIO ULIMWENGU TUNAOISHI
article-2303428-003641A200000258-193_638x416.jpg


SENGWILE MAKAMANDA
Deadbody
Dunia zaidi ya tuijuavyo
 
Back
Top Bottom