Mejasoko
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 298
- 595
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Karagwe.
____
1. Tundu Lissu siyo Donald Trump. Wanafanana ukali wa maneno lakini hawafanani ujinga wa kisiasa. Wote walipigwa risasi, zikawaongezea kura zao.
2. Lissu ni hukumu isiyo na rufaa kwa watawala wanaotumia risasi badala ya hoja. Rudisheni risasi mfukoni, nendeni shule mjifunze hoja. Wamarekani walitumia risasi, sasa wanaongozwa na “kichaa mstaarabu”.
3. Tundu Lissu siyo Trump. Kwa Trump mihimili inajitegemea na ina nguvu katika kufanya kazi. Hapa kwetu, mihimili inategemea kusemwa na kusimangwa ndipo ifanye kazi.
4. Mmemsahau Spika Makinda? “Mwanangu Lissu, hebu tusaidie tunaondokaje hapa”. Natamani Tulia atulie mbele ya Makinda apate twisheni ya kufanya kazi na Lissu.
5. Lissu na Freeman wameelewana, lakini wapambe wao wamenuniana. Tatizo lilikuwa moja; Lissu aliwamudu wapambe wake; Freeman wapambe walimmudu.
6. Yaliyotokea ni somo kwetu: Wapambe wa Lissu waliweza kumuambia ni wakati gani sahihi wa kuingia uwanjani, lakini wapambe wa Freeman hawakuweza kumwambia ni wakati gani sahihi wa kutoka uwanjani.
7. Kama kuna makosa yoyote Freeman aliyafanya kwa muda wa miaka 21 aliyoongoza Chadema, basi makosa yake yote ameyafuta kwa kubonyeza kitufe kimoja tu: kuendesha uchaguzi kwa uwazi na kukubali matokeo.
8. Lissu kachukua 'mkopo mkubwa’ na wenye riba kubwa sana, lakini kazungukwa na vibaka. Je atamudu kurejesha mkopo huo?
9. Neno langu kwa Mbowe: Umejenga heshima kubwa, umeondoka kwa heshima kubwa. Ilinde heshima hiyo. Ukistaafu, staafu.
10. Neno langu kwa Lissu: Mahaba ya kutongozea ni tofauti na mahaba ya kuishi na mke katika ndoa. Jitathmini.!