Lissu tuambie, unaamini Bunge la sasa linaweza kufanya maboresho ya sheria ya vyama vya siasa,uchaguzi na katiba mpya?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,038
4,752
Tunakubaliana wote yaani CCM na upinzani kwamba Bunge la sasa halina uhalali kutokana na uharibifu uliofanywa kwenye uchaguzi 2020.

Tunakubaliana wote kwamba dhamira ya Mhe. Rais aitengenezi vifungu vya sheria Bali inaweza Tu kufungua milango Kwa mabadiliko ya sheria.

NI wazi kabisa kwamba hakuna kiongozi ndani ya Bunge lililopo ambaye amewahi kuona tatizo ya sheria ya uchaguzi wala kukubali kwamba uchaguzi 2020 ulibakwa.

Kwa spirit hiyo hiyo naamini tunakubaliana kwamba Bila Bunge la vyama vingi nivigumu kuwa na sheria inayolinda maslahi ya vyama vingi.

Tunakubaliana kabisa kwamba hata kipindi tunatafuta demokrasia ya vyama vingi si maono ya viongozi wala wananchi yaliyoonekana kukubaliana na vyama vingi Bali maono ya Mwalimu Nyerere ambaye alivuka hata kuyapindua maono ya Mzee Mwinyi wakati huo.

Nazionea huruma Kodi za wananchi katika mchakato huu; nazionea huruma nikitaka hata akina Tundu Lisu wazionee huruma na kulishauri Taifa lisitumie fedha Kwa mambo yasiyo zaa tija. Naomba wenyeviti WA vyama vya upinza na wenza wao watusaidie kujibu swali

NI Bunge gani litaratibu mabadiliko kuelekea katiba mpya?
 
Back
Top Bottom