Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 19,803
- 21,815
CHADEMA iko dhaifu kama ilivyo, na inaendelea kudhoofika, kumong'onyoka na kugawanyika vipande vipande kwa haraka sana, kwa sababu ya manguli hawa wawili waandamizi, kila moja anajigamba kwamba ndie mwenye nguvu zaidi ya mwingine, ama ndie mwenye sauti.
Haki ya nafasi au cheo fulani, ushawishi na wafuasi wengi zaidi ya mwingine hali inayosananisha mvutano wa ndani kwa ndani.
Mambo haya hayasemwi lakini yapo ndani ya CHADEMA, yanafukuta na yanafanyika kimya kimya na kila upande ukiogopa na kuoinea haya, aibu na wivu upande mwingine. Na miongoni mwa wanaopata tabu zaidi Kisiasa mioyoni mwao, ni wale amabao wamejizuia, wamejitenga au hawajaamua wawe upande gani kati ya upande wa Mwemyekiti au Makamu Mwenyekiti taifa.
Soma Pia:
Hawa, wamekua wapweke, wamaekua kama yatima ndani ya chama chao wenyewe, walichokijenga kwa moyo, hali na mali, na kukipigania kufa na kupona kwa muda mrefu sana. Wengi wao hivi sasa, wameshaanza kuhamia vyama vingine vya Kisiasa, na wengine wengi kwa maelfu yao wanatafakari na kujipanga kufanya hivyo hivyo, endapo mafahali hawa hawatabanduka kwenye nafasi zao au kumaliza mivutano yao ya chini kwa chini na kubadilika.
Kisiasa,hata kama aking'atuka moja wao pekee, na mwingine akabaki uongozoni, bado hali ya cold war yani vita baridi ndani ya CHADEMA na hasa miongoni mwa pande za mafahali hawa wawili kuhujumiana itaendelea CHADEMA, na kwahivyo, chama kitaendelea kuteketea na kua dhaifu zaidi kadiri siku, miezi na miaka inavyosonga.
CHADEMA inahitaji damu mpya, fikra pevu mpya, uelekeo, mawazo, mipango, maono na pumzi mpya kuimarika tena na kua na nguvu. Vinginevyo hali hii ya kutokuaminiana au kutokua na uhakika hata ya nani atakua Mgombea Uraisi wake Uchaguzi ujao, itaendelea kukigharimu, kukipasua zaidi chama hicho na kuwatia hofu Wanachama wake.
Haya ni maoni na mtazamo wangu kitaalamu juu ya Siasa za CHADEMA kwa uchache sana.
unafikiria nini kuhusu mustakabali wa baadae wa Siasa za chama hicho?
MUNGU IBARIKI TANZANIA

CHADEMA ndani Kwa ndani kunafukuta
Ndani ya chadema ni mvurugano tu, wapo walio bora na wasio bora, ndiyo shida kuu!