Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,513
- 3,771
Akihojiwa na BBC Swahili, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amewashangaa wanaodai kuwa hafai kuongoza hata Mtaa wakati kitambo kidogo alifaa hadi kuwa Rais (Akapewa dhamana ya kugombea Urais) na pia amefaa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA
Amesema “Huyu Lissu ambaye hafai kabisa kuwa Mwenyekiti alikuwa anafaa kuwa Rais, in fact alikuwa anafaa kuwa Makamu wa Mwenyekiti. Ukiwa Makamu Mwenyekiti, Mungu akifanya mapenzi yake na tukasema Bwana Ahimidiwe, Makamu ndio anakuwa Mwenyekiti”
Amesema kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA ‘is a heartbeat away’ kuwa Mwenyekiti, kuwa Moyo wa Mwenyekiti ukizima kwa mapenzi ya Mungu, Makamu Mwenyekiti ndio anakuwa Mwenyekiti.
Ameongeza kuwa mtu anayesema ‘hufai kabisa’ kama ingekuwa mazingira mengine ungemuuliza ‘wewe kichwa chako kipo sawa?’ Ila kwa sababu ni mazingira ya Uchaguzi unaelewa.