Lissu jifunze, Huwezi kushika dola kwa kupambana na dola, Never

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
22,220
49,597
Lissu sio mwanasiasa haijui siasa kaingia kwenye siasa ili kufanikisha malengo yake ya uanaharakati.

Lengo la mwanaharakati sio kushika dola ni kutetea haki na kuleta mageuzi, tofauti na lengo la mwanasiasa ambalo ni kushika dola.

Mbowe ni mwanasiasa, mwanasiasa makini hutumia hoja, dialogue, ballot box kushika dola na anaweza kuvumilia hata miaka 50, tofauti na mwanaharakati anayetaka shortcut kutimiza malengo yake iwe kwa mapambano au hata kumwaga damu.

Lissu anatakiwa apate washauri wazuri wa siasa atofautishe siasa na uanaharakati, asijifananishe na akina Maria Sarungi ambao hawana dhamana ya wanachama wanaweza kusema chochote na wasihojiwe na yeyote.

Awe na uvumilivu, aambiwe hawezi kupambana na dola akabaki salama vile vile aambiwe huwezi kupambana na boss wako ukabaki salama.
 
Lengo la mwanaharakati sio kushika dola tofauti na lengo la mwanasiasa ambalo ni kushika dola.

Mimi hadi sasa sijaona mahali lisu anapambana na mwenyekiti wake na ninafuatilia speech zake vizuri kabisa anaongea maneno ya busara tuu! ila ninacho kiona ni wapambe na wafuasi wa ccm wenye malengo yao hasi ndio wana kuza na kmuwekea maneno lisu
 
Wanaharakati ndio wanaleta vuguvugu mabadiliko duniani kote. Baadaye kukiwa na misingi bora, mizuri kama katiba mpya, uchaguzi huru ndio siasa inafanyika kwa uhuru, haki na uwazi.

Kupinga na kutokomeza utumwa, uhuru wa nchi mbalimbali, haki kwa watu weusi, haki za wanawake vyote vilianzishwa na wanaharakati kwanza.

Baadaye kupitia siasa zikatengenezwa sheria kulinda haki mwanzo ilikuwa harakati za watu wachache.
 
Sawa, fanya hilo vuguvugu pasipo kukivuruga chama unachotegemea kuja kushika dola.
Kusema kuna watu wanakula Pesa za Abdul ndio kukivuruga Chama?

CHADEMA ilikua na misingi iyo tangu zamani, kukemea rushwa na kupambambana na mafisadi, leo hii akigusia swala la rushwa ndani yya chama amevuruga chama? Sasa hapo kuna chama au wachunia tumbo tu kama wenzao wa kijani

Kuna watu wamekufa kwa kupambania chama wakiamini wapo kwenye harakati za ukombozi, kumbe wakubwa juu wanakula meza moja na mafisadi ya kijani

Asingesema Lissu haya yote tusingeyajua, sasa tumejua hatuwezi kudanganywa tena.

Sasaivi mtu mpumbavu tu ndio ataweka maisha yake rehani kisa CHADEMA
 
Nchi zote duniani zilipata Uhuru na Dola kwa uanaharakati.

Acha uongo.
Ni kama hujui Historia

Vyama vya upinzani haviwezi kushika Dola bila harakati kama hakuna uwanja sawa.

Nchi zenye demokrasia ndio hakuna vyama vya siasa venue harakati kwa sababu kuna uwanja sawa baina ya vyama.
 
Kusema kuna watu wanakula Pesa za Abdul ndio kukivuruga Chama?

CHADEMA ilikua nanmisingi iyo tangu zamani, kukemea rushwa nankupambambana na mafisadi, leo hii akigusia swala la rushwa ndani yya chama amevuruga chama? Sasa hapo kuna chama au wachunia tumbo tu kama wenzao wa kijani

Naona wameishaisahau hotuba ya Dr Slaa Mwembeyanga list of shame kuhusu ufisadi bila kuogopa wala kupepesa macho iliyowapa CDM umaarufu mkubwa na kuwa kimbilio la Watanzania.

CDM waliwataja kuanzia Rais, Waziri mkuu, Kikwete, Mkapa, Lowassa,Mkono, Karamagi, Balali, Mramba, Chenge, Rostam Aziz, Mgonja mafisadi papa wengine, Mapapa walioshika dola.

Chadema ilipambana na dola bila kupepesa macho, kwa ujasiri mkubwa na harakati za kila aina.

Harakati zilizaa matunda makubwa. Tanzania ilikuwa karibu kupata katiba mpya, tume huru, na sheria za kudhibiti mafisadi na ufisadi.
 
Mimi hadi sasa sijaona mahali lisu anapambana na mwenyekiti wake na ninafuatilia speech zake vizuri kabisa anaongea maneno ya busara tuu! ila ninacho kiona ni wapambe na wafuasi wa ccm wenye malengo yao hasi ndio wana kuza na kmuwekea maneno lisu
Hujamsikia akisema Mbowe anatumia michango ya chama kwa maslahi yake.
 
Watanzania wengi ni wanafiki na wanapenda unafiki nafiki tu. Mtu akiwa mkweli kanyooka, lazima wamchukie na kumtungia kila aina ya ubaya. Lissu ndiyo mtu sahihi kwa wakati huu. Tanzania inahitaji mtu mwenye kaliba ya TAL.

Mtu asiseme ukweli eti anapambana na dola, mnapenda kusikia uongo na kudanganywa kama watoto. Mtu asigombee eti anapambana na boss wake. Boss who? Hiko chama mtuambie ni cha familia,ccm ama ni kanyaboya tu. Kama ni chama cha upinzani, yeyote mwenye sifa atagombea mtake msitake.
 
Kusema kuna watu wanakula Pesa za Abdul ndio kukivuruga Chama?

CHADEMA ilikua na misingi iyo tangu zamani, kukemea rushwa na kupambambana na mafisadi, leo hii akigusia swala la rushwa ndani yya chama amevuruga chama? Sasa hapo kuna chama au wachunia tumbo tu kama wenzao wa kijani

Kuna watu wamekufa kwa kupambania chama wakiamini wapo kwenye harakati za ukombozi, kumbe wakubwa juu wanakula meza moja na mafisadi ya kijani

Asingesema Lissu haya yote tusingeyajua, sasa tumejua hatuwezi kudanganywa tena.

Sasaivi mtu mpumbavu tu ndio ataweka maisha yake rehani kisa CHADEMA
Chama huendeshwa kwa misingi ya katiba, kanuni na miiko hata kama umeona tatizo kuna taratibu zake za kuhoji na sio kuropoka.
 
Lissu sio mwanasiasa haijui siasa kaingia kwenye siasa ili kufanikisha malengo yake ya uanaharakati.

Lengo la mwanaharakati sio kushika dola tofauti na lengo la mwanasiasa ambalo ni kushika dola.

Mbowe ni mwanasiasa, mwanasiasa makini hutumia hoja, dialogue, ballot box kushika dola na anaweza kuvumilia hata miaka 50, tofauti na mwanaharakati anayetaka shortcut kutimiza malengo yake iwe kwa mapambano au hata kumwaga damu.

Lissu anatakiwa apate washauri wazuri wa siasa atofautishe siasa na uanaharakati, asijifananishe na akina Maria Sarungi ambao hawana dhamana ya wanachama wanaweza kusema chochote na wasihojiwe na yeyote.

Awe na uvumilivu, aambiwe hawezi kupambana na dola akabaki salama vile vile aambiwe huwezi kupambana na boss wako ukabaki salama.
R.i.p JONAS SAVIMBI..
 
Lissu sio mwanasiasa haijui siasa kaingia kwenye siasa ili kufanikisha malengo yake ya uanaharakati.

Lengo la mwanaharakati sio kushika dola ni kutetea haki na kuleta mageuzi, tofauti na lengo la mwanasiasa ambalo ni kushika dola.

Mbowe ni mwanasiasa, mwanasiasa makini hutumia hoja, dialogue, ballot box kushika dola na anaweza kuvumilia hata miaka 50, tofauti na mwanaharakati anayetaka shortcut kutimiza malengo yake iwe kwa mapambano au hata kumwaga damu.

Lissu anatakiwa apate washauri wazuri wa siasa atofautishe siasa na uanaharakati, asijifananishe na akina Maria Sarungi ambao hawana dhamana ya wanachama wanaweza kusema chochote na wasihojiwe na yeyote.

Awe na uvumilivu, aambiwe hawezi kupambana na dola akabaki salama vile vile aambiwe huwezi kupambana na boss wako ukabaki salama.
Sasa Lisu ni tofauti kabisa , kesi za mchongo sio rahisi kufanikiwa kwake kwa sababu hafanyi jambo lolote nje ya katiba na sheria.
Tundu Lisu Ana moyo wa haki .Tundu Lisu ni muwazi , muadilifu na anaichukia Rushwa kwele kweli .
Kwa uadilifu wa Lisu ni wazi kuwa ana kibali mbele za Mungu kwa ajili ya kuijenga Tanganyika yenye haki katikati ya rasilimali nyingi alizoziumba Mungu kabla ya Kuwepo kwa CCM na Chadema . Tundu Lisu amesimama na wananchi katika kupigania maisha ya wengi
 
Mtu pekee anaweza kumtingisha kama si kumchomoa mother ni Lissu tu,Mbowe mama uhakika mpaka 2030.

Kusoma hamjui hata kuona TU nako hamuoni?
Nakubaliana na wewe, lkn siasa zina taratibu zake ambazo lazima zifuatwe tofauti na uanaharakati ambapo mtu yeyote anaweza from nowhere akalianzisha au akaamua kuingia msituni.
 
Mtu pekee anaweza kumtingisha kama si kumchomoa mother ni Lissu tu,Mbowe mama uhakika mpaka 2030.

Kusoma hamjui hata kuona TU nako hamuoni?
Unajua Samia anajua hataweza kusimama na Lissu kwenye kampeni.

Samia hana uwezo wa kujieleza, hana mafanikio yoyote, rekodi yoyote muhimu ya kuboresha maisha ya Watanzania zaidi ya udalali wa maliasili.

Anaweza kujivunia maridhiano, kuua chama kikuu cha upinzani kwa rushwa.

Mpinzani wake mkuu kwa sasa ni Lissu, anatumia na atatumia kila namna kumdhibiti, kumfunga mdomo. Atatumia hata vyombo vya dola kumdhibiti ndiyo namna pekee ya yeye kushinda bila shida yoyote.

Mbowe hana madhara yoyote kwake, infact ni swahiba wake,ndio maana walimpa tuzo, akawapa 150m kupitia Mbowe kwa kanisa. Na sasa hivi kamati kuu ya CDM ipo chini ya Abdul kupitia wenje kuwapa bahasha.
 
Lissu sio mwanasiasa haijui siasa kaingia kwenye siasa ili kufanikisha malengo yake ya uanaharakati.

Lengo la mwanaharakati sio kushika dola ni kutetea haki na kuleta mageuzi, tofauti na lengo la mwanasiasa ambalo ni kushika dola.

Mbowe ni mwanasiasa, mwanasiasa makini hutumia hoja, dialogue, ballot box kushika dola na anaweza kuvumilia hata miaka 50, tofauti na mwanaharakati anayetaka shortcut kutimiza malengo yake iwe kwa mapambano au hata kumwaga damu.

Lissu anatakiwa apate washauri wazuri wa siasa atofautishe siasa na uanaharakati, asijifananishe na akina Maria Sarungi ambao hawana dhamana ya wanachama wanaweza kusema chochote na wasihojiwe na yeyote.

Awe na uvumilivu, aambiwe hawezi kupambana na dola akabaki salama vile vile aambiwe huwezi kupambana na boss wako ukabaki salama.
Anawalaza bila viatu, ndio maana mmelambisha Mbowe asali ampungyze Lissu makali

Bahati mbaya sana mtaendelea kuchumwa na mishale yake
 
Mbowe ni mwanasiasa, mwanasiasa makini hutumia hoja, dialogue, ballot box kushika dola na anaweza kuvumilia hata miaka 50, tofauti na mwanaharakati anayetaka shortcut kutimiza malengo yake iwe kwa mapambano au hata kumwaga damu.
Mbona kashinda mitaa 20 tu nchi nzima na huo so called uanasiasa? Hata Trump was against the system ila ameshinda, same to Ruto!! Hayo mambo don't matter kwa Tanzania maana hakuna demokrasia. Meaning unahitaji mtu radical kama Lissu au Heche ili walete amsha amsha hadi CCM ikubali mabadiliko ila tukiendelea na hao moderates kama Mbowe tutaendelea tu kupewa jimbo moja tu mengine wapewe CCM alafu tunaitwa mezani.
 
Unajua Samia anajua hataweza kusimama na Lissu kwenye kampeni.

Samia hana uwezo wa kujieleza, hana mafanikio yoyote, rekodi yoyote muhimu ya kuboresha maisha ya Watanzania zaidi ya udalali wa maliasili.

Anaweza kujivunia maridhiano, kuua chama kikuu cha upinzani kwa rushwa.

Mpinzani wake mkuu kwa sasa ni Lissu, anatumia na atatumia kila namna kumdhibiti, kumfunga mdomo. Atatumia hata vyombo vya dola kumdhibiti ndiyo namna pekee ya yeye kushinda bila shida yoyote.

Mbowe hana madhara yoyote kwake, infact ni swahiba wake,ndio maana walimpa tuzo, akawapa 150m kupitia Mbowe kwa kanisa. Na sasa hivi kamati kuu ya CDM ipo chini ya Abdul kupitia wenje kuwapa bahasha.
1. Nimeahangaa mnoo Mbowe kumuweka Wenje mbele ilhali ni mtuhumiwa wa rushwa

2. Mbowe amekuwa kipofu totoro
 
Back
Top Bottom