Kwa Mara nyingine tena Mbowe na Tundu Lissu wameingia kwenye mzozo mwingine ikiwa ni siku moja tu tokea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kutangaza ziara katika kanda ya Kaskazini ambayo ililengwa kuwa na mikutano zaidi ya 104 katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha,Tanga na Manyara.
Ziara ambayo ilitangazwa itakuwa ni ya siku 21 katika majimbo 35 tayari imeshaingia dosari siku ya pili tu tokea kuanza kwa ziara Makamu Mwenyekiti Tundu Lisu ameisusia ziara hiyo kwa madai kuwa Mwenyekiti amejipanga kwa bajeti kubwa ikiwa yeye ametoka kwenye ziara katika mkoa wa Singida bila ya kuwa na bajeti iweje Mbowe afanye kufuru.?
Siku ya jana baada ya kumalizika kwa mikutano ilibidi yeye na delegation yake ikiongozwa na Askofu Mwanamapinduzi wajigharamie Chakula na Malazi kitu ambacho Lissu alikipinga na hakikuwa katika ratiba yake.
Hali hiyo ilimlazimu Tundu Lissu achukue sehemu ya michango aliyochangiwa na wanaharakati pamoja na diaspora kununulia gari kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni 2 kulipia malazi tu hali ambayo imemkasirisha Makamu Mwenyekiti na kupelekea kususia ziara hiyo kwa madai kuwa yeye hana pesa na alikwenda kwenye hiyo ziara kwa mualiko wa Mwenyekiti wake.
Tundu Lissu anasema kuwa Mbowe alipaswa kumuhudumia kama Kiongozi yeye pamoja na delegation yake lakini ilipofika jioni baada ya kumaliza mikutano kila mtu anashika njia yake kitu ambacho kimemfanya Tundu Lissu aingie mitini kuendelea na ziara.
Tunaposema Lissu na Mbowe hawapikiki tena chungu kimoja ni wazi sasa hivi imebakia kugawana magwanda tu na kila mmoja kushika njia yake.
Kwaheri Lissu.
---
JamiiCheck.com imefuatilia hoja hii na kuja na majibu. Soma hapa chini:
- SI KWELI - Tundu Lissu kaenda kutibiwa Ulaya