Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,422
- 35,202
Nimekuwa nikifiatilia kauli za Lissu mara kadhaa na kujikuta nabaki na mshangao mkubwa.
Lissu mara kadha amekuwa akiwashambulia viongozi wenzake ndani ya chama bila ushahidi wenye mashiko.
Kelele za fedha za Abdul na Mama Abdul zimekuwa silaha kubwa ya Lissu kupigania nafasi ya Mwenyekiti taifa.
Mwanzoni mtuhumiwa mkuu alikuwa Wenje lakini baadae akapanua uwigo wa kuwaingiza viongozi au wanachama wote wasiokuwa upande wake.
Kabla habari za fedha za Abdul na Mama yake hazijapoa kaja na taarifa za aliyempatia habari kuhongwa viongozi wa Chadema ni Mjumbe wa Kamati Kuu lakini sasa ni Marehemu !.Hapo hapo hataki kumtaja jina kawaachia kitendawili chepesi mashabiki wake.
Lissu ni mwanasheria anajua kumtaja jina mhuhusika (Marehemu) kungemlazimisha kisheria kuitwa kutoa ushahidi.Alichokifanya ni kutoa maelezo ambayo wafuatiliaji au mashabiki wataelewa mhusika ni nani bila kuumiza akili lakini hapo hapo bila kulazimika kuingia katika mitego ya kisheria.
Pengine hii naweza kusema hapa ndipo ilipo tofauti kubwa baina ya Lissu na Lyatonga Mrema.Huwezi kumshtaki kwasababu hajataja jina wala sababu za kifo lakini hapo hapo anaendelea kumchafua mpinzani wake ndani ya chama pengine mpinzani wake mwingine nje ya chama (anatengeneza mtaji wa mashabiki)
Week moja iliyopita alikuja na suala la yeye kuumizwa na serekali halafu zigo adondoshewe Mbowe.Karejesha fomu za kugombea uenyekiti huku kavaa nguo za kujikinga na risasi.Hiyo ni sehemu ya kampeni ndani ya chama na nje ya chama.
Mpaka tarehe 25 Jan 2025 nategemea washindani wake wengi ndani ya chama (FAM) na nje ya chama (Mama Abdul) watakuwa wamevurumishiwa zigo la tuhuma za kutosha.
Ngongo kwasasa Kogatende.