Huyu Odemba anamzuia mtu kuzungumza, anadhani yupo hapo kushindana na wale anaowahoji, matokeo yake anageuza kipindi chake kuwa kijiwe cha wapiga soga, aambiwe aache huu ushamba.
Kwa upande mwingine kuhusu hoja ya mahesabu iliyoibuliwa na Msigwa, kisha kupigiwa kelele na wasiompenda Mbowe.
Hivi kama Chadema kuna upotevu wa pesa, CAG hajawahi kukagua huko? kama anakagua, kwanini asiseme upotevu upo badala yake Chadema imekuwa ikipata hati safi karibia kila mwaka chini ya Mbowe wasiemependa?
Huyu Msigwa amekuwepo Chadema miaka yote, lini amewahi kuzungumzia hilo jambo ndani na nje ya vikao akiwa Chadema?
Kwanini azungumze sasa baada ya kuondoka? nikisema huko kuzungumza kwake ni matokeo ya zile script anazoandaliwa na kina Dr. Nchimbi azungumze, kama tulivyoona siku ile akitambulishwa nitakuwa nakosea wapi?!
Haya madai ya upotevu wa pesa yamejaa siasa tu, kama yupo mwenye ushahidi wa wizi kwanini anaukalia asiuweke hadharani? mnaogopa nini?
Ok, Mrema na Mnyika wanaogopa kusema ukweli kama mnavyotaka kutuaminisha, vipi na CAG nae anaogopa?
Ni ajabu sana ngoma inayopigwa na CCM, kuona wakata viuno wake wako Chadema.