The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,611
- 3,442
Kwa muhitasari:
Tundu Lissu: "Ni rafiki yangu wa muda mrefu tangu mwaka 2006. Kuhama kwake kumeniumiza sana na ni pigo kwa chama kwa sababu Msigwa alikuwa ni mtu mpamnaji mzuri sana"
Tundu Lissu: "Kwa kuwa alikuwa ni rafiki yangu ktk misingi ya harakati za mapambano ya kisiasa na kwa kuwa keshahamia kwenye kambi ya maadui zetu kisiasa, huo ndiyo mwisho wa urafiki wetu"
Tundu Lissu: "Angeniambia kuwa anahamia CCM, bila shaka tungegombana sana maana nisingetegemea aniambie kitu hicho"
Pia soma: Lissu athibitisha kuandika barua ya kugombea Urais, asema CCM wameweka fedha katika Akaunti yake, tatizo liko wapi?
Tundu Lissu "Mimi kuhamia CCM labda niwe sina akili. Siwezi kushirikiana na hawa madalali wa rasrimali za nchi yetu, wezi na mafisadi. Narudia, mimi kuhamia CCM nikiwa na akili zangu timamu hivi, ni ndoto za mchana...!"
Kwa uhondo zaidi, sikiliza na kumtazama video clip hii mwenyewe hadi mwisho.