figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,671
- 55,579
Lipumba alipaswa kufanya nini kama alikusudia kutaka kurejea katika nafasi ya Uenyekiti?
SEHEMU YA PILI: [FACTS FINDING] Katiba ya CUF;
Na. Maharagande,
“….Kutokana Na [IQ-Intelligence Quotient] ndogo ya baadhi ya hawa wenzetu waliopata elimu kupitia Programu ya MEMKWA itabidi twende taratibu kwa muundo wa maswali na majibu [FACTS FINDING] ili dozi iingie uzuri…” na sasa tunaendelea sehemu ya pili kama ifuatavyo:
QUESTION NUMBER 8:
Je kuandika barua tu ya KUSUDIO LA KUJIUZULU hakumfanyi kiongozi kuwa kajiuzulu mpaka mamlaka yake ya uteuzi/uchaguzi ikubali kwa mujibu katiba ya CUF?
COUNTER:
JIBU NDIO. Kusudio la kujiuzulu kwa sharti la Tarehe ya kujiuzulu ipo mbele ya wakati na muhusika anaendelea na utekelezaji wa wajibu wake, hakumfanyi muhusika/kiongozi kuwa amejiuzulu kwa wakati huo. Katiba ya CUF inaelekeza kuwa kujiuzulu kwake kutatimia mpaka mamlaka ya uteuzi au uchaguzi ikubali. Lakini sharti hili halifanani hata kidogo na jinsi Lipumba alivyofanya.
Ingekuwa sawa kama mathalani Barua ya kujiuzulu kaiandika Tarehe 5/8/2015 kisha akaainisha kuwa IFIKAPO Tarehe 5/2/2016 [katika kipindi cha miezi 6 baadae] nitajiuzulu. Hii ndio inaitwa [KUSUDIO LA KUJIUZULU-NOTICE OF INTENTION TO RESIGN/NOTICE OF RESIGNATION] hapo Katibu wa mamlaka [Maalim Seif] kupitia Baraza Kuu la Uongozi la Taifa angepaswa aandae Mkutano Mkuu wa Dharura wa Taifa kujadili hilo. Na pia kama pasingekuwepo na Mkutano Mkuu ulioandaliwa mpaka KUFIKIA Tarehe 5/2/2016 angehesabiwa kuwa amejiuzulu nafasi yake Tangu Tarehe hiyo 5/2/2016. Kumbuka kuwa Ibara ya 117(1) haimlazimishi kiongozi kuendelea na nafasi ya uongozi. Katiba imempa Haki ya kujiuzulu. Haki hiyo haiwezi kupokonywa au Ibara nyingine ya Katiba.
QUESTION NUMBER 9:
Je ni kweli kwamba Lipumba mpaka Tarehe 21/8/2016 wakati Mkutano Mkuu Maalumu unaitishwa alikuwa ni Mwenyekiti wa CUF kwa mujibu wa katiba ya CUF?
COUNTER:
HAPANA. Hakuwa Mwenyekiti wa CUF kwa rejea ya majibu ya Q&C Number 4, 5, 6 and 7 herein above.
QUESTION NUMBER 10:
Je katiba ya CUF imempa mamlaka kiongozi wa CUF kutengua maamuzi yake? Kama alivyofanya Lipumba Tarehe 6/6/2016 kuandika barua ya kutengua kujiuzulu?
COUNTER:
HAPANA. KATIBA HAIJARUHUSU KIONGOZI ALIYEJIUZULU KUTENGUA KUJIUZULU KWAKE, bali mamlaka hayo yamewekwa katika Ibara ya 79(1) (f) Rejea Q&C Number 1 hapo juu. Lakini Pili, Katiba Ibara ya 117(2) imeweka utaratibu na hatua zinazopaswa kuchukuliwa pindi Kiongozi anapojiuzulu. NI VIKAO NDIVYO VYENYE MAAMUZI SI MUHUSIKA MWENYEWE [ALIYEJIUZULU]
QUESTION NUMBER 11:
Je wakati lipumba anajiuzulu alikuwa anasubiri majibu ya barua yake? Kama alivyoeleza hapa “…kwa kuwa barua yangu ya Tarehe 5/8/2015 haijajibiwa nimeamua kuitengua na kurejea kwenye nafasi yangu nilichaguliwa ya Mwenyekiti wa Taifa…” !!!!!!!!! hahahaaa Je hili linakubalika Kikatiba?
COUNTER:
HAPANA. Alipoandika BARUA YA KUJIUZULU Tarehe 5/8/2015. Hakudai kwamba anasubiri majibu ya kukubaliwa au kukataliwa. Tarehe 6/8/2015 alikwenda Peacock Hotel akaongea na waandishi. Akataja sababu za kujiuzulu ikiwemo NAFSI NA DHAMIRA YAKE IMEMSUTA. Akapanda gari. Akaenda Airport. Akaelekea KIGALI, RWANDA. Kufanya utafiti wa Uchumi. Ili kuja kuisaidia kuishauri serikali ijao baada ya uchaguzi [hakutaja itakuwa ya chama gani], Hakushiriki katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu. Wala hakushiriki katika KUPIGA KURA. Hakuandika barua ya kusudio la kujiuzulu bali aliandika barua ya KUJIUZULU. Na ALIPOFUATWA KUOMBWA ASIJIUZULU ALIKATAA. Rejea majibu Q&C number 5 and 6 herein above.
QUESTION NUMBER 12:
Je kiongozi aliyejiuzulu na kukaa miezi 12 [mwaka mmoja] nje ya ofisi ya kazi na kusimama kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba, anaweza kuanza tena ‘RASMI’ shughuli zake ndani ya ofisi hiyo kwa kigezo cha kumuandikia barua Katibu Mkuu pekee?
COUNTER:
HAPANA HAIRUHUSIKI. Katibu Mkuu hana mamlaka kwa mujibu wa Katiba ya CUF Ibara ya [81(2), (a)] [93(1) (f)] [85(4)] na Ibara ya 118 kwa sababu Taarifa za Kujiuzulu kwa Lipumba zilishafikishwa kwa ngazi hizo za vikao na kufanyiwa maamuzi. Miongoni mwa maamuzi ya vikao hivyo ni;
Moja; Baraza Kuu liliundaa Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa kwa lengo la kusaidiana na Katibu Mkuu kuratibu shughuli za Chama katika kipindi cha Mpito kuelekea kujazwa kwa nafasi wazi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti waliojiuzulu. Kamati hiyo ya watu Watatu iliongozwa na Twaha Issa Taslima na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini kabla ya ‘kurukwa na fahamu’ alipokea Taarifa ya Chama na kumtambua rasmi na kufanya nae kazi mbalimbali.
Maamuzi ya Baraza Kuu yamezingatia Ibara ya 101(1) ya Katibu ya CUF inaeleza wazi kwamba “ Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linaweza, pindi likiona inafaa, kuanzisha Kamati, Tume au Taasisi yoyote ile ya Kitaifa yenye lengo la kusaidia utekelezaji mzuri wa sera na itikadi za Chama, au kufanya uchunguzi juu ya jambo lolote lile linalohitaji
kufanyiwa uchunguzi.”
Pili; Baraza Kuu lilishatoa ratiba ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Taifa kujadiliwa na kujazwa kwa nafasi hiyo.
Tatu: Lipumba alipojiuzulu kwa kutambua kuwa yeye si Mjumbe tena wa Baraza Kuu hakuweza kuhudhuria vikao zaidi ya vitatu vya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa. Je? kama inadaiwa bado alikuwa ni Mwenyekiti halali Katiba Ibara ya 122 (1) na (2) inaeleza nini kwa mjumbe asiyehudhuria kikao kinachomuhusu?
ITAENDELEA SEHEMU YA TATU……………….
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
Maharagande,
DECEMBER 28, 2017