Wataalamu wa sayansi ya saikolojia wanashauri nini hapa. Tuhuma za usaliti hazikomi. siamini kabisa kama ana amani moyoni, na kwa umri alionao sasa naona kama ameporomoka ghafla. Sioni kama heshima yake ipo tena. Kifo cha rakiki yake naona kimemnyanganya heshima yake yote. Ana uwezo wa kukemea lolote na taifa hili likatetemeka kwa sauti yake. Baada ya mzee wa Lupaso taifa lilibaki na yeye. Baada ya msiba huu anaweza kufyoka kweli wajumbe wakaufyata kama alivyokuwa yule mzee wa Lupaso. Kuna haja ya kurudisha heshima yake, nini kifanyike sasa ili irudi. Mbali na Rais lazima awepo mzee mwenye sauti akiongea Raisi anashituka, wajumbe wanashituka, bunge linashituka. Kwa namna hali ilivyo hana uwezo baada ya heshima yake kuporoka ghafla kule Monduli. Wataalamu ya Sayansi ya siasa kwa afya ya taifa wanashauri nini kifanyoke kurudisha heshima yake katika taifa hili. INadhani hata Ile remote aliyosema Roma Mkatoriki betri zitakuwa zimeisha na hata zikibadilishwa kutakuwa na kutu tayari.