Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,870
- 5,045
Wapiga kura wapya 102,668 wanatarajiwa kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura Manispaa ya Lindi kupitia zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa taarifa za wapiga kura lililoanza Januari 29 hadi Februari 3,2025 Mkoani Lindi.
Uandikishaji huo kwa upande wa Manispaa ya Lindi ni kwa majimbo mawili ya uchaguzi,Jimbo la Mchinga na Lindi Mjini ambapo kwa mujibu wa Afisa mwandikishaji Mkuu wa daftari hilo Juma Mnwele, Jimbo la Mchinga wanatarajia kuandikisha wapigakura 43,547 huku Lindi mjini wakiandikishwa 59,121.
Mapema Januari 29,2025 Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Zuwena Omari na Mkuu wa Wilaya hiyo Victoria Mwanziva wameungana na wananchi wa kata ya Mtanda kujiandikisha huku viongozi hao kwa pamoja wakitumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi hilo ili itakapofika mwezi Oktoba wapate fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani.
Manispaa ya Lindi inajumla ya vituo 245 ambavyo vinatumika kuandikisha wananchi wenye sifa ikiwemo waliotimiza umri wa miaka 18.
Wengine ni wapiga kura ambao wanarekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine,kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania au kifo.
Pia, Soma: