Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,504

Star wa muziki nchini Marekani Lil Wayne ameshambuliwa kwa mara nyingine tena na ugonjwa wa kifafa.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, ndege binafsi aliyokuwa amepanda rapper huyo, ililazimika kutua kwa dharura huko Omaha, Nebraska Jumatatu hii. Weezy alikuwa akisafiri kutoka Milwaukee kwenda California pindi tukio hilo lilipotokea.
Wayne alidaiwa kuzimia akiwa kwenye ndege na kupewa huduma ya kwanza. Hata hivyo ripoti zimedai kuwa alikataa kutibiwa. Taarifa zimedai kuwa alipata tena kifafa cha pili baada ya ndege yake kupaa na ililazimika arudishwe Omaha. Alipoteza kabisa fahamu na alipelekwa hospitali kwa ambulance.
Tunechi aliwahi kupata tatizo kama hilo mwaka 2012 baada ya ndege binafsi kutua kwa dharura kwa siku mbili mfululizo.
Pia aliwahi kupata kifafa kikali mwaka 2013.