Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,499
- 121,191
Wanabodi,
Hili ni bandiko mwendelezo wa three series za uchambuzi wangu wa sheria mpya ya Uchaguzi, 2023. Kama hukuona 1st series, anzia hapa Asante Rais Samia kwa Muswada huu. Umuhimu wa mabadiliko ya Katiba kabla ya Sheria hii bado ni muhimu sana. Huu ni uchambuzi Wangu - Part 1 kisha uje hapa
Asante Rais Samia kwa Muswada huu. Umuhimu wa mabadiliko ya Katiba kabla ya Sheria hii bado ni muhimu sana. Huu ni uchambuzi Wangu - Part 1
Kisha Je Wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni Batili?. Ni Mvinyo wa Zamani, Kwenye Chupa Mpya?. Why Ubatili Huu?!.
Pia unaweza kupita hapa Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!. na hapa Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?.
Binadamu tuna mtindo wa kuangazia mapungufu zaidi na kujikuta tunakuwa blinded na mapungufu hivyo kutoona mazuri, hata kwenye Biblia ukitaja tuu jina la Yuda, mind za wengi zinakwenda kwa usaliti wa Yuda Iskariote, kumbe kwenye watumishi wa Yesu, kulikuwa na Yuda wawili, Yuda Iskariote msaliti na Yuda Tadei mtu mwema. Jina la Yuda limeghubikwa na usaliti hadi wema wa Yuda Tadei kufunikwa na usaliti wa Yuda Iskariote.
Ndivyo ilivyo hii sheria mpya ya uchaguzi, kufuatia sheria hii kuletwa na ubatili ule ule tunaoupigia kelele kila uchao, tunajikuta tunakuwa too blind to see mema na mazuri ya muswada huu
Hivyo leo naendelea na uchambuzi wangu wa kifungu hadi kifungu huku nikiainisha the good, the bad and the ugly.
Karibu.
Leo naendelea na uchambuzi wangu wa muswada huu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023, kwa mukhtaasari wa sura zote 10 za sheria hii, kuwaelimisha elimu ya uraia na elimu ya sheria na haki ili Watanzania tuitumie kikamilifu hii miezi 3 ya kutoa maoni na mapendekezo ya maboresho ya sheria hii.
Muswada huu unatunga Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani ya mwaka, 2023. Kwa ujumla, Sheria hii inaunganisha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292. Hivyo sasa masharti ya uchaguzi wa Rais na Wabunge na Madiwani ni sheria moja na kutekelezwa na mamlaka moja ambayo ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hapa ninapendekeza chaguzi zote nchini, uchaguzi wa Rais na Wabunge, Madiwani na Serikali za Mitaa, ufanyike siku moja na kusimamiwa na Tume moja Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hili ni jambo jema!.
Wiki iliyopita nilichambua sura ya kwanza mpaka ya tatu, leo naendelea
Sura ya Nne ya Muswada inaweka masharti yanayosimamia uchaguzi wa Wabunge na imegawanyika katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza inahusu sifa za wagombea katika uchaguzi wa Ubunge. Sehemu ya Pili inahusu uteuzi wa wagombea Ubunge ambapo inaainisha siku ya uteuzi, uteuzi wa wagombea, utaratibu wa namna ya kuweka dhamana kwa mgombea wa nafasi ya ubunge, masharti ya mgombea kuteuliwa kwa jimbo moja tu, pingamizi na uamuzi juu ya uhalali wa fomu ya uteuzi
Sura hii pia inaainisha utaratibu wa kufuatwa endapo kuna mgombea mmoja tu halali wa nafasi ya ubunge au endapo hakuna mgombea. Kwa mujibu wa Sehemu hii endapo kutakuwa na mgombea mmoja halali wa nafasi ya Ubunge ameteuliwa, mgombea huyo atapaswa kupigiwa kura na atatangazwa kuwa amechaguliwa endapo atapata kura nyingi za ndiyo kati ya kura zote halali zilizopigwa
Maoni: Hili ni jambo jema, zuri na lenye maslahi kwa taifa kwa kurejesha mamlaka kwa wananchi, sasa hakuna tena ushindi wa mtu kupita bila kupingwa!. Kupita bila kupingwa kulifanya chama kuwachagulia wananchi kiongozi. Hii itaondoa zile figusu za kuzuia watu wasigombee, kuwanunua wapinzani na kuzuia fomu zisirejeshwe na mtu kutangazwa mshindi wa kupita bila kupingwa!. CCM ina wabunge 18 ambao wamepita bila kupingwa!.
Sura ya Tano ya Muswada inahusu masharti ya uchaguzi wa Madiwani. Sura hii imegawanyika katika Sehemu Tatu, ambapo Sehemu ya Kwanza inabainisha masharti ya uendeshaji wa uchaguzi wa madiwani, muda wa kuwa madarakani kwa Madiwani, namna na wakati wa kuitisha uchaguzi mdogo na uwakilishi katika Kata. Sehemu ya Pili inaweka masharti kuhusu sifa za mgombea na mazingira ya mtu kukosa sifa ya kuteuliwa katika uchaguzi. Sehemu ya Tatu inajumuisha masharti kuhusu siku ya uteuzi, uteuzi wa mgombea, dhamana za wagombea, utaratibu wa kuweka pingamizi na utaratibu unaopaswa kufuatwa ikiwa kuna mgombea mmoja tu wa nafasi ya udiwani au ikiwa hakuna mgombea.
Sura ya Sita ya Muswada inaweka masharti kuhusu uchaguzi, utaratibu wakupiga kura na uteuzi wa wabunge na madiwani wanawake viti maalum. Sura hii imegawanyika katika Sehemu Sita, ambapo Sehemu ya Kwanza inaweka masharti mbalimbali kuhusu siku ya uchaguzi na tangazo la uchaguzi. Kwa mujibu wa masharti hayo, taarifa ambazo zitakuwa katika tangazo la uchaguzi ni pamoja na siku na muda wa kuanza na kufunga upigaji kura, anwani ya vituo vya kupigia kura, wapiga kura waliopangwa kwa kila kituo cha kupigia kura na taarifa za wagombea walio teuliwa kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi. Sehemu ya Pili inaweka masharti kuhusu mgombea kujitoa na utaratibu unaopaswa kufuatwa endapo mgombea atafariki au hakuna mgombea. Sehemu ya Tatu inaweka masharti kuhusu kampeni za uchaguzi na namna kampeni zinavyopaswa kuendeshwa, ikiwa ni pamoja na masharti kuhusu kuwasilisha ratiba ya mikutano kwa msimamizi wa uchaguzi kwa lengo la kuepuka migongano ya mikutano. Sehemu hii inaweka pia masharti kuhusu upatikanaji na wajibu wa vyombo vya habari vya umma na matakwa ya kutokuwa naupendeleo na kuepuka ubaguzi kwa mgombea yeyote katika utoaji wa matangazo.
Maoni: Hapa bado kuna tatizo, mgombea mmoja ana ving’ora, ana media team ya serikali, ana PA ya serikali, ana magari ya serikali na watendakazi wa serikali!. Nchi za wenzetu, rais aliye madarakani anapongombea tena, anakuwa scrapped off all presidential privileges isipokuwa ulinzi na wale wagombea wengine wote wa urais wanapatiwa ulinzi na basic logistical support kama ni ving'ora, wote ni ving'ora na sio utaratibu wetu wa mgombea mmoja mwenye dola ameshika mpini kugombea kisu cha makali kuwili na wagombea makapuku!, unategemea ushindani wa haki?.
Sehemu ya Nne ya Sura hii inaainisha utaratibu wa uchaguzi unaojumuisha masharti kuhusu siku na muda wa kupiga kura, mawakala wa upigaji kura, masanduku ya kura, muundo wa karatasi za kura na katazo la kuweka wazi kura.
Sehemu ya Tano inaweka masharti kuhusu utaratibu wa kupiga na kuhesabu kura. Masharti hayo yanajumuisha watu wanaostahili kupiga kura, mazingira yanayoweza kumfanya mtu kupotezasifa za kupiga kura, utaratibu wa kupiga kura, watu wanao ruhusiwa kuingia katika kituo cha kupigia kura, mazingira yanayoweza kusababisha kuahirishwa kwa upigaji kura inapotokea vurugu, kufungwa kwa zoezi la upigaji kura na utaratibu wa kuhesabu kura. Kwa mujibu wa masharti ya Sehemu hii, mawakala wa upigaji kura wanatambuliwa kuwa mawakala wa kuhesabu kura. Vilevile Sehemu hii inaainisha wajibu wa msimamiziwa kituo baada ya kuhesabu kura, utaratibu wa kujumuisha kura katika uchaguzi wa wabunge na madiwani na utaratibu wa kutangaza matokeo ya ubunge na udiwani. Sehemu ya Sita ya Sura hii inaweka masharti kuhusu uteuzi wa wabunge na madiwani wanawake viti maalum na unatambua utaratibu ulioainishwa katika Katiba na Sheria za Serikali za Mitaa kuhusu wabunge na madiwani wanawake viti maalum.
Itaendelea wiki ijayo.
Wasalaam
Paskali