RASCO BOY
JF-Expert Member
- Jul 29, 2018
- 428
- 485
June 31, 2007.. Raisi wa Zamani wa Libya Hayati Moummar Gadafi akiwa amesindikizwa na walinzi qake wa kike Waaminifu alihutubia ktk Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) jijini Accra- Ghana huku akiwa amevalia Shati lake la khaki lenye picha za Wapiganaji na waasisi wa mataifa ya Afrika wenye Misimamo Mikali (Pan Africansts) kama Patrice Lumumba, Abdul Naser, julius kambarage Nyerere, kwame Nkurumah, Nelson Mandela, Sekou Toure, Thomas Sankara n.k.
Ndani ya mkutano Gaddafi akasema "Ndugu zangu Waafrika, tunapaswa Kuchagua Moja aidha kuiunganisha Afrika yetu au kuruhusu ife tunapaswa kuwa na muungano wa Mataifa ya kiafrika na kuunda (United States of Africa) tuna kila kitu ndani ya bara hili sasa ni vema tukaitimiza Ndoto hii kwa kuwa Wamoja tunaweza kupambana na Ulimwengu wa kileo"
Ndipo miaka kadhaa baadae Gaddafi ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Afrika Mstaaff (AU) alivamiwa pale Libya.. akauawa pale pale Libya kwa kile kilichopambwa na Mabeberu huko Ulaya na Amerika kwa neno "DIKTETA" neno ambao Mara zote Mabeberu na Vibaraka wamekuwa wakilitumia dhidi ya Viongozi wote wa Mataifa Machanga wanaojaribu kujinasua ktk Mtego wa Ukoloni wa kiuchumi.
Kabla ya kuuawa kwa Gaddafi Libya ilikuwa na Fedha Nyingi kuliko idadi ya wananchi wake, Walikula na kusaza na hata Fedha nyingine zikaelekezwa kuufadhili Umoja wa Afrika (AU) posho zote za vikao na mishahara ilitoka Libya Mbali ya maendeleo Afrika Nzima, Mabilioni ya Dollar yakatumika kumaliza Ghasia za vita kule Niger na Mali, Baadhi ya misaada tuliyopata Tanzania kama Nchi ni pamoja na Kujengewe Msikiti pale Dodoma.
Leo Raia wa Libya wanasaga meno kwa Upumbavu wao, waliyakataa Maisha ya kifahari waliyoishi, Maisha ya kupewa Mishahara bila kufanya kazi kupewa mke na kulipiwa mahari na hata kupewa nyumba uanze Maisha....Leo wana Laana na Damu ya Gaddafi na Chozi la Gaddafi juu ya Ardhi yao ni wapi kwenye Raha? Sirte? Tripoli au Benghazi?... Vurugu tupu.
Tumpende na Tumuunge mkono Raisi wetu Magufuli hatatupa maisha bora na yenye furaha tumpe muda watanzania tuache kukariri Tumepata Raisi anayewarenga hao unaowaona kwenye picha katika shati la shujaa Gaddafi.....
Ni hayo Tu
Sent using Jamii Forums mobile app