Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,430
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekemea tabia ya baadhi ya viongozi kujichukulia sheria mkononi ikiwamo kuwapiga wananchi wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa ya kituo hicho kwa vyombo vya habari jana, iliyotiwa saini na Mkurugenzi Mtendaji wake, Anna Henga, hali hiyo inadidimiza ustawi wa haki za binadamu.
“Ni wazi kuwa tabia ya viongozi katika ngazi mbalimbali kujichukulia sheria mkononi imeshamiri hususani vitendo vya vipigo kwa wananchi wenye tuhuma za makosa ya jinai. Hali hii inazidi kudidimiza ustawi wa haki za binadamu.
“Pia inadidimiza misingi ya utawala bora nchini kwa mujibu wa viwango vya kimataifa hususani mkataba wa haki za kiraia na kisiasa wa mwaka 1966 pamoja na kitaifa kama ilivyowekwa katika Katiba,” iliema taarifa hiyo.
Kituo hicho kilitoa wito kwa serikali kuchukua hatua za makusudi kudhibiti vitendo hivyo.
“LHRC inatoa wito kwa serikali kuchukua hatua za makusudi kudhibiti vitendo hivyo ikiwamo kukemea, kusimamisha, kutengua, uteuzi wa viongozi mara moja pale yanapotokea matukio ya aina hiyo. Tuhuma zozote za makosa ya jinai au madai zinapaswa kuwasilishwa katika vyombo vya kisheria.
“Ibara ya 13 ya Katiba inaweka haki kwamba watu wote ni sawa mbele ya sheria na wana haki ya bila ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa. Inaeleza wazi kuwa ni mahakama pekee ndicho chombo cha utoaji haki, viongozi na wananchi wana jukumu kubwa la kulinda amani ya nchi kwa kufuata sheria na Katiba walioapa kuilinda,” iliongeza taarifa hiyo.
Pia LHRC ilimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Harrison Kamoga, kwa kuchukua hatua ya kumsimamisha kazi Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Hydom, aliyemshambulia mwananchi.
Mtendaji huyo wa kijiji aliyefahamika kwa jina la Adella Kente, anadaiwa kumshambulia mwananchi wa kijiji hicho cha Hydom, Rose Danielson, Januari 12, mwaka huu, kwa tuhuma za kutolipa michango ya kijiji.
Matukio ya baadhi ya viongozi kuwachapa hadharani watu wanapokosea yamekuwa yakisambaa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni.
Hivi karibuni, kwa mfano, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kennan Kihongosi, aliwachapa viboko wananchi na wazazi wa watoto waliodaiwa kuiba vifaa vya ujenzi wa shule na madawati na kufanya chuma chakavu.