Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,136
- 1,956
Taarifa ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ya kulaani mauaji ya watu Watatu wa familia moja huko Dodoma imesema, hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko kubwa la matukio ya kikatili nchini hususani ya mauaji, watu kupotea na kutekwa ambayo yanaongeza hofu kubwa kwa wananchi kwani yanatishia usalama wao na jamii nzima
Taarifa hiyo imeeleza, ongezeko la matukio haya pia kwa sehemu yanaashiria udhaifu wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambayyo jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kunakuwepo na ulinzi thabiti wa raia na mali zao
Kupitia taarifa hiyo LHRC imetoa wito kwa Mamlaka husika kuchunguza tukio hilo na kubaini chanzo cha mauaji, kisha kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria