Leo nimepita pale gairo kwenye kiwanja cha shule ya msingi,, kumejaa watazamaji kulikuwa na mechi ya cricket nikapata fikra india imehamia tanzania!!!

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,602
2,055
Kwa yeyote anayehusika na uhamasishaji, ufuatiliaji , utaratibu na uratibu wa kusimamisha, upatikanaji wa uwanja, uboreshaji wa uwanja huo na upatikanaji wa timu.

Mafunzo ya timu hizo, mpaka kuwezesha kufanyika law mashindano madogomadogo ndani ya wilaya ya GAIRO.

Tumezoea kushuhudia , uanzishwaji wa timu za mpira wa miguu lkn hapa GAIRO imekuwa tofauti muitikio umekuwa mkubwa kwa vijana kujitokeza kujifunza mchezo wa CRICKET.

Siyo kila eneo la dunia hii ni maarufu kwa mchezo wa SOKA! , maeneo mengine yanajitabanaisha kwa kuwa maarufu kupitia michezo mingine ambayo wanavipaji navyo lkn kutokana na kutokuwepo kwa fursa za uwepo wa viwanja na vifaa vya mchezo husika na mafunzo vipaji hupotea.

Soka ni mchezo mama ambao ndani yake vipaji vingine HUIBUKA. Kwa yule aliyeamua na kujitolea GAIRO isimame na CRICKET , MUNGU MUWEZA WA YOTE AMUANGAZIYE.

Wengine nendeni ndani ndani huko , kuna vijana wazuri wenye vipaji vya michezo mbalimbali kama NGUMI, RIADHA, BADMINTON NK.

DAR imejaa mno, ujanjaujanja mwingi vipaji na umakini uko kijijini. Unayeamua kusimamia hili nenda mwenyewe huko ukiweka CHAWA ujue utalia na KULAUMU.

LEO nimepita pale GAIRO kwenye kiwanja cha shule ya Msingi,, kumejaa watazamaji kulikuwa na mechi ya CRICKET nikapata fikra INDIA imehamia Tanzania!!! KUMBE yawezekana tukawa MABINGWA WA DUNIA kwa mchezo wa CRICKET.
 
Back
Top Bottom