Habari za siku waheshimiwa wana jukwaa,natumai Mungu anaendelea kuwalinda na kuwaongoza katika familia zenu na katika shuguli zenu za kila siku.Nitumie nafasi hii ya siku ya kuzaliwa kwangu ambapo natimiza miaka 33,kuwatakieni pia amani na upendo katika familia zenu na bidii katika ufanisi wa kazi zenu kwa manufaa ya familia zenu.Mwisho nawaomba tuombeane katika siku hii ya leo mwenyezi mungu atubariki sote na pia familia yangu,wanangu methew na moses na pia mrs wangu Rehema mwenyezi MUNGU awanyoshee mkono wake katika ukuaji wao wa kiroho.MUNGU AWABARIKI SANA.KARIBUNI