Kumbe huyo mumeo alikua amesha ujua mchezo ulio mfanyia, kwa maelezo alio nieleza nikwamba wewe ulimdanganya kwamba mimi ni Rafiki wako kikawaida tu, tena akaniambia kwamba umempa na sim ambayo mimi nilikupa wewe, na kumbe ulisahau kufuta conversation zangu mimi na wewe hapo ndipo alipo anza kuisoma picha nzima.
Nakumbuka kipindi kile mama alinipigia sim kwamba amepigiwa sim na mwanaume alie jitambulisha kwamba ni mumeo na mimi ninamchukulia mkewe, tena jamaa alienda mbali na huku akimwambia mamaangu kwamba ataniua, sikuhiyo mamaangu alifadhaika sana na alinipigia sim kuniuliza mambo yale yalivyo.Then niliamua kudanganya mama kwamba huyo ni mtu mwenye wivu wa kimapenzi tu, na hiyo nilifanya ili nimpoze mamaangu kwa kuogopa presha isije ikapanda na tuka taabika sisi wanawe.
Anyway.....
Hili jambo nilikaa nalo moyoni kwa muda na tayari upendo wangu kwako ulitoweka na nilianza kusubiri tu muda ufike nikuje Tz ili tumalize jambo lile, hivyo nikaamua kuvumilia.
Nilipo rejea Tz, tulizungumza na ulijitetea sana huku ukilia machozi kwamba nikusamehe kwakua jamaa alikurubuni na huku ukisingizia kwamba ulipitiwa na shetani pia kishawishi.
Nilikuomba tuzungumze na huyo mumeo ili tuweke mambo sawa ili kila mmoja akue na amani na maisha yaendelee, ukweli niliumizwa sana na tukio lile na nilikujibu kwamba sikupendi tena na sina hisia na wewe tena, nilikusisitiza kwamba wale watoto wako wawili wanao soma na wakwangu nitaendelea kuwalipia ada kama kawaida na nitawapa mahitaji kama pale mwanzo.
Hii picha ilikua haijifuti akilini mwangu hasa pale ulipokua umechanuliwa miguu.
Hatimae nilirejea hukooo duniani kuendelea na kibarua kama kawaida.
Baada ya muda kiasi kupita niliamua kuanzisha mahusiano na mdada mwingine hapa jf huku tukiwa kwenye mazungumzo na kweli nilimueleza kwamba nilikua na wewe ingawa ndio tulikua kwenye harakati za kamba kukatika.
Bidada aliridhia na nilibakiza zoezi la kukuacha rasmi.
Nikiwa kwenye harakati za kukuacha ghafla skumoja uliniambia habari kwamba mumeo yule wa kwanza ulie zaa nae amemuagiza mwanao akuje kwako kipindi cha likizo, hapo nakumbuka wanangu pamoja na wanao wote walikua likizo na wote ulikua nao hapo jijini.
Then nikasema poa hakuna shaka kwakua baba wa huyo mwanao wa kwanza amemuagiza mtoto sikuona tatizo, lakini nilipata wazo la kuku track down ili niweze ziona calls, MMS na SMS zote zinazo ingia kwako.
Hapo ndipo tena nilipo ona maajabu....
kumbe huyo mumeo wa kwanza alikuja hapo jijini, na wewe ndie ulie lipia hotel kwakua alikuambia hana pesa, na pia ukalala nae pale hotel kisha kesho ukarudi na mwanao kule ulipo kua ukiishi.
Aiseeee.....
Ingawa nilikua nimekueleza kwamba sina mapenzi na wewe na sijutaki tena, ila niliumia sana kwamba natoa pesa mimi alafu wanaume wengine ndio huzitumia...!!