ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,318
- 50,529
Weekend iliyopita nilikuta watoto wanavua samaki baharini karibu na mapango ya mawe Mida ya saa tano maji yalipokuwa yanajaa. Ikanivutia sana nikaomba nitengenezewe ndoano moja nikajaribu na mimi kuvua ila sikubahatika kupata samaki wale madogo walipata pata sasa nimekaa chini nimefikiria kwanini nisiunde ndoano nyingi ndefu hata 10 kisha niziunganishe halafu niwe naenda kuzitega kama wanavyozitega wale wavuvi wa maji malaini ya mitoni.. Asubuhi naenda kuzicheki unaweza ukakutana na bonge moja la kitoewo.. Maisha ni akili hata chalamila yuko sahihi hela inategwa sometimes na bahati hela inahusika hela/mafanikio haitafutwi Kwa pressure sana.Nitaleta mrejesho nikiwa na picha za ndoano.