greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,653
- 3,009
Leo naomba nitoe elimu fupi Juu ya Hisa,,,,Hisa ni nini,faida yake ni ipi na mtu unawezaje kushiriki....
Karibuni katika Darasa hili by Mwalimu Architect
Kabla ya kwenda moja kwa moja kwenye Hisa,hebu tujuzane juu ya Kampuni.
1.
KAMPUNI : Ni biashara iliyo sajiliwa kisheria kwa ajili ya kutoa huduma. Ambapo kuna aina kuu mbili za kampuni kulingana na aina ya umiliki
Sasa hapo kwa nadharia ya Hisa,
Lakini hiyo kampuni ya umuiliki wa ushirikiano,upo wa aina mbili.
PRIVATE LIMITED/UMILIKI BINAFSI : Kwenye aina hii ya kampuni ni ina umiliki binafsi,ina kiwango cha idadi ya wamiliki mara nyingi haitakiwi wazidi watu 200.
2.
KAMPUNI KWANINI KAMPUNI IWE PLC (PUBLIC LIMITED COMPANY)
3.
SOKO LA HISA
4.
FAIDA YA USHIRIKI
Karibuni katika Darasa hili by Mwalimu Architect
Kabla ya kwenda moja kwa moja kwenye Hisa,hebu tujuzane juu ya Kampuni.
1.
KAMPUNI : Ni biashara iliyo sajiliwa kisheria kwa ajili ya kutoa huduma. Ambapo kuna aina kuu mbili za kampuni kulingana na aina ya umiliki
- SOLE PROPPRIETOSHIP/UMILIKI WA PEKEE ,Hii ni biashara/Kampuni inayo milikiwa na mtu mmoja tu.Unapo sajili biashara yako ya duka ama stationary na kujiweka wewe pekee kama mmiliki ndipo unakuwa umefanya usajili huu.
- PARTNERSHIP/USHIRIKIANO: Hapa umiliki unakuwa ni wa watu wawili au zaidi.
Sasa hapo kwa nadharia ya Hisa,
- SOLE PROPPRIETOSHIP/UMILIKI BINAFSI: Hii ni kampuni ambayo inakuwa na Mwanahisa mmoja tu.
- PARTNERSHIP/USHIRIKIANO: Hii ni kampuni ambayo jnakuwa na wanahisa kuanzia wawili na kuendelea.
Lakini hiyo kampuni ya umuiliki wa ushirikiano,upo wa aina mbili.
PRIVATE LIMITED/UMILIKI BINAFSI : Kwenye aina hii ya kampuni ni ina umiliki binafsi,ina kiwango cha idadi ya wamiliki mara nyingi haitakiwi wazidi watu 200.
- Hailazimishwi kisheria kuchapisha taarifa zake za fedha na uendeshaji.
- inaweza ikawa ina milikiwa kifamilia,kindugu
- Kampuni nyingi kubwa hapa Tanzania zipo kwenye mfumo huu,hasa za watanznia wa asili ya Asia
- Kampuni lazima ichapishe taarifa zake za fedha za mwaka mzima ili umma uweze kuzipitia.
- ambapo kwa Tanzania kuna makampuni 26 tu yenye aina hii ya umiliki wa kampuni.
- Sasa hapa kwa hesabu fupi ina maana kampuni yenye wamiliki 400 itakuwa na hisa 400,kwasasa tuishie hapo
2.
KAMPUNI KWANINI KAMPUNI IWE PLC (PUBLIC LIMITED COMPANY)
- Upatikanaji wa mtaji : kampuni inaongeza mtaji wake kupitia ununuzi wa hisa zake.
- Ufanisi ,ina saidia kuongeza ufanisi katika kampuni,kwani taarifa zake zitakuwa zina chapishwa na kila mtu anaweza kuziona.
- Kutumika kama dhamana na rahisi kuaminika kwenye kuomba mikopo.
3.
SOKO LA HISA
- Unakumbuka juu ya hesabu yetu ya wamiliki 400,sawa na hisa 400.
- sasa Kampuni kulingana na ukubwa wake,hufanyika hesabu na kuona iwe na idadi flani ya Hisa.Sasa utakuta kuna kampuni ina jisajili kuwa ina hisa Miliion 2.Hapo sawa na wamiliki million 2.
- lakini huwa hakuna kizuizi cha idadi ya hisa ambazo mtu anaweza kununua,mtu mmoja anaweza kumiliki hisa 100,mwengine 50 hapo uwezo wa mtu binafsi kuweza kumiliki.
- Ila kadri unavyozidi kuwa na Hisa nyingi ndipo nguvu yako ndipo inapokuwa kubwa kwenye maamuzi ya kampuni.
- Kuna hesabu hufanyika na kuamua thamani ya kila Hisa moja ya kampuni husika.
- Kuna kampuni inaweza kuwa na bei ndogo ya hisa ila ikawa na idadi kubwa ya hizo mf.CRDB ila kuna kampuni hisa zai zake ni gharama ila idadi ndogo za hisa mf.TBL na TCC
- Kununua/Kuuza hisa ni kununua sehemu ya umiliki wa kampuni.
- Hii hufanyika katika soko maalum,ambapo kwa Tanzania ni Soko la hisa la Dar.
- Kampuni inaweka Hisa Sokoni,mwananchi unazinunua
- Ukinunua hisa ni zako milele,labda mpaka ikatokea kampuni ikafirisika.
- Lakini nawe unaweza ziweka sokoni na kuziuza
4.
FAIDA YA USHIRIKI
- Kufanya biashara ya kuuza na kununua hisa.
- Kupata gawio la mwaka,pindi kampuni inapotengeneza faida.
- Sehemu ya kuzuia kuporomoka kwa thamani ya fedha,kwakuwa hili ni soko,napo bei za hisa huweza kupanda kutokana kupanda kwa inflation.Hisa iliyouzwa 200 mwaka 2010 ,sasa itakuwa 400 ,so thamani ya hela yako inakuwa imelindwa.
- Unaweza kuzitumia kama dhamana katika kupata mikopo.
- Hali kuwa mmiliki wa wa kampuni/kushiriki vikao vya mwaka/kupiga kura/kujuana na watu.
- Pakua/download app ya HISA KUGANJANI/DSE
- Jaza taarifa zako
- utapewa CDS number
- Chagua wakala wako/BROKER
- Fanya uchambuzi wa kampuni unayotaka kununua hisa zake
- nunua hisa
- Unaweza shiriki masoko ya hisa ya nchi mbali mbali duniani...ila anza na la Nyumbani kwanza.
- Ni vizuri kufanya uchambuzi kwanza
- Anza na kununua hisa chache.
- Usinunue hisa za aina moja tu ya biashara,mana sekta hiyo ikikumbwa na msukosuko basi kampuni zo huko zote hushuka kithamani i.e Hisa zisiwe za mabenki tu.
- CMSA : Ndiyo mamlaka inayosimamia uendeshaji masuala yote ya Soko la hisa....
- Kampuni nzuri kwa kununua hisa kwasasa ni TWIGA,CRDB,NICOL....kwa mtaji mdogo
- kama una mtaji mkubwa nunua hisa za TCC na TBL