Wakuu, leo nimesononeshwa mno na hali niliyokutana nayo ndani ya mgahawa mmoja hivi ambapo siku za nyuma (Takribani miezi miwili iliyopita) nilipita hapo kunywa cha kwa Tshs 400. Hii ilikuwa ni kawaida kwa kipindi kirefu kwani nimekuwa nikipita kwenye mgahawa huu mara kwa mara nisafiripo nje ya kituo cha kazi.
Lakini cha kushangaza leo napita sehemu ileile na kuuziwa kikombe kilekile cha chai kwa Tshs 1000. Kuhoji nikaambiwa kuwa sukari wanauziwa bei ya ghali mbaya zaidi kwa shida mno! Huu ni mfano dhahiri wa serikali iliyo madarakani kushindwa kwa kiwango kikubwa kuwatumikia wananchi waliyoiweka madarakani!
Nimejiuliza sana ni nini hasa faida ya kuwa na chombo kinachoongoza nchi na kwakweli nimeshindwa kuziona. Kama jambo dogo la sukari serikali inashindwa, vipi kwa jambo kubwa?
Nimetafakari sana ni watanzania wangapi wanaweza kumudu hili ndani ya nchi yao! Mbaya zaidi ukihoji unakumbana na dola iliyosheheni nguvu, hili ndiyo hasa halikubaliki! Wananchi tuna haki ya kuhoji na kupewa ufumbuzi pale ambapo mambo hayaendi ipasavyo.
Tunaiomba serikali ijikite kushughulikia kero za kila siku za wananchi. Wananchi wanatakiwa kuona fahari wawapo ndani ya nchi yao maana wanaitumikia na kujitolea kwa kila hali kuijenga. Tusiwaache wananchi wakalia ndani ya mioyo yao huku tukiwa na uwezo bado wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo tena mapema kabisa.

Ilikuwa 1800 sasa hivi baadhi ya maeneo ni sh.6000,hapo unatarajia wauze ah.ngapi mkuuWaluiziwa Sh ngapi sukari kiasi cha kikombe cha chai kupandishwa kwa sh 600?
Uongo mwingine muwe mnawadanganya barvicha wenzenu
Kwa hiyo kilo ya sukari ni kwa watu kumi?Ilikuwa 1800 sasa hivi baadhi ya maeneo ni sh.6000,hapo unatarajia wauze ah.ngapi mkuu
Ulitegemea bei elekezi iwe constant?nackia bei elekezi now ni 2200,nayo imepanda
mbn hamna mahali nlipouliza mkuu?angalia vizuriUlitegemea bei elekezi iwe constant?
Mbona bei elekezi ya mafuta huulizi??
We ch.izi soma uelewe! Kabla ilikuwa inauzwa 400 kwa kikombe na sasa ni 1000 ikimaanisha bei imepanda kwa 600 na hii ni kutokana na ukata wa sukari na bei kuwa juu. Haijalishi itakuwa hotelini au kwa mama ntilieMuwe mnasoma kabla hamjaingia,ili mjue hiyo ni hotel,café,motel,restaurant au mama ntilie....tafuta hadhi yako.