Lengo lako la kujiunga JF limefanikiwa?

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
8,142
22,021
Kuna ambao wamejiunga na huu mtandao wakiwa na lengo maalumu wengine imetokea tu wapo hapa bila sababu. Je ulijiunga JF ukiwa na lengo gani? Umefanikisha kilichokuleta kwenye huu mtandao?

Sikumbuki vizuri nimejiunga lini JF ila nafikiri nipo hapa kwa miaka minne au mitatu. Binafsi kilichonileta hapa ni mapambano ya kusaka connection za kazi/vibarua. Ieleweke sio kwamba nililidhika na hali ya ujobless na kukaa tu ndani, nimekua nikifanya vibarua vya kunipa hata hela ya kusurvive ila ni wajibu wa kila mtu kutafuta kazi ya taaluma aliyosomea tunaangukia tu huku kwingine baada ya game kuwa tough.

Kwa kipindi hicho nilikua natumia facebook na instagram tu lakini niliona sio platform sahihi kwa lengo langu kutokana na kujaa vijana wengi ambao bado wanajitafuta na wenye kasumba ya kupenda showoffs mitandaoni. Nikaona nielekeze nguvu jamiiforums na linkedin. Jf nilikua naijua kabla ya hapo ila linkedin ilikua ndio mara yangu ya kwanza kuitumia.

Kwa kuzingatia wabongo ni watu wanaopenda kutukuzwa na kunyenyekewa hasa akiwa amekuzidi umri au cheo ikanilazimu niwe naandika na kuchangia mambo positive, ikanilazimu ni-fake personality yangu nikiwa kwenye keyboard kwa kujifanya mtu mwema sana (mimi sio mtu mbaya lakini kama binadamu kila mtu ana dark side yake).

Kwa kipindi chote nipo hapa jf sijawahi kupata connection ya kazi wala kibarua chochote zaidi ya motivational speechs tu, speechs ambazo nimeshazizoea na hazinisaidii chochote katika harakati za mkono kwenda kinywani.

Naweza kusema lengo la mimi kuwa hapa halijafanikiwa vipi wewe mwenzangu lengo lako la kujiunga jf limefanikiwa?
 
Ulijiunga JF 25 March 2020.
Sasa kama taarifa nyepesi namna hii tena zinakuhusu zinakutatiza, mambo makubwa ya connection utayaweza kweli Mkuu?

Binafsi nimepata mambo mengi zaidi ya niliyoyatarajia hapa JF.
Kwani si nimekadiria hapo kwa kusema ni miaka minne au mitatu. Hujui makadirio?. Kama utajari tunaomba utuambie ukijiunga kwa malengo gani na ukitumia mbinu zipi kufanikiwa uenda kuna wenye malengo kama yako wanaweza kufaidika
 
Kwani si nimekadiria hapo kwa kusema ni miaka minne au mitatu. Hujui makadirio?. Kama utajari tunaomba utuambie ukijiunga kwa malengo gani na ukitumia mbinu zipi kufanikiwa uenda kuna wenye malengo kama yako wanaweza kufaidika

Nimekuelewa, lakini kukadiria kitu ambacho taarifa zake unazo au unaweza kuzipata sio jambo zuri sana, hiyo itakusaidua huko mbele ya safari.

Nikimuuliza kwanini umepata muda wa kuandika vizuri bandiko refu na ukakosa muda wa kuangalia profile Yako ulijiunga lini ukaamua kukadiria utakua nayo?

Tukirudi kwenye hoja ya msingi, nilijiunga JF niweze kupata mambo mbali mbali yanayojiri hapa kwetu na duniani Kwa ujumla. Lakini pia niweze kutoa maoni yangu na kushiriki mijadala mbali mbali. Mwisho JF ni burudani tosha kwangu na sehem ya kutoa stress kwa kusoma maoni ya wanachama.
 
Back
Top Bottom