Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,690
- 14,001
Habari zenu wanaJF wenzangu,
Baada ya kufuatilia kwa makini vile vinavyozungumziwa na makamu mwenyekiti wa Chadema mhe Tundu Lisu, nimegundua kwamba jamaa amejipanga kujaribu kuuwa ndege wawili kwa wakati mmoja ili aweze kufanikiwa lengo lake la muda mrefu, japo inaonekana wazi kuwa kwa aina ya ndege anaotaka kuwaangusha, hakuna ndege hata mmoja ambae ataweza kumdondosha kwa namna yoyote ile itakayojaribu kuitumia.
1. Tukianza na ndege namba moja (mkuu wa wakuu wote)
Ndugu Lisu amekuwa akijaribu kupambana na mkuu huyu kwa kujaribu kumchafua kwa kumtupia lawama mbali mbali za kweli na zisizokuwa za kweli, ilimradi afanikiwe kumchafua, kumdhalilisha, kumvunja moyo na kumfanya aonekane hafai mbele ya wale anaowaongoza akiwemo yeye mwenyewe Lisu.
Kwa bahati mbaya au nzuri watanzania wa leo sio wale wa enzi za mwembeyanga, Soweto Arusha nk. Wa leo wengi wanajitambua na kuelewa kila kitu. Unaweza kuongea utumbo wako wakakupuuza na kukuacha uendelee kubaki na utumbo wako hivyo hivyo, au wengine wakaonesha kuunga mkono utumbo wako, lkn wakakupa adhabu kubwa katika sanduku la kura na kukufanya ubaki unalalamika mwenyewe.
2. Ndege namba mbili (namba moja wa chama chake)
Bila shaka ameshaona kuwa namba moja wa chama chake sio mpinzani wa kweli, ni mchumia tumbo anaeweka masilahi ya tumbo lake na familia yake mbele (kumbuka sakata la Lowasa), hivyo kwa yeye (namba 1 wake) kuendelea kuwa kitini kama kiongozi, ni njia moja wapo inayosababisha chama chao kishindwe kushika dola. Hivyo anajaribu kutupa makombora ambayo yatakuja kumsaidia yeye kupata uungwaji mkono wa kugombea unamba moja wa chama hicho hapo baadae (miezi kadhaa iliyobaki).
Mfano ameanza kuhoji aliemualika mkuu wa wakuu katika kilele cha siku ya wanawake duniani (happy woman's day) mwaka jana. Bila shaka anajua wazi ni nani alietoa wazo, au ruhusu ya mkuu huyo wa wakuu kualikwa, lkn kwa kuhofia kutengwa na chama chake katika uchaguzi ujao, ameshindwa kumface namba 1 wake huyo wa chama, na badala yake ameishia kuzungumka mbuyu kwa kuhoji aliemwalika adui yake (mkuu wa wakuu)
Pili ameanza kulalamika kuwa kuna pesa za mama Abdul (mkuu wa wakuu) zinatumika kupitisha watu wa kukiangamiza chama. Bila shaka ameshamjua mtu ambae aliwahi kwenda katika "jumba la taifa" kinyemela zaidi ya mara mbili kuonana na huyo mama Abdul (mkuu wa wakuu) bila kuwataarifu wenzake na wakapanga waliyoyapanga bila mtu mungine kinyume na waliokuwepo huko kujua kilichozungumziwa na kupangwa.
Hii inaonesha wazi kuwa huenda mhe Lisu sasa anataka kujitokeza kugombea unamba 1 wa chama ili akipeleke chama hicho kwa style ile anayotaka yeye kiende. Ila anahofia pesa za mama Abdul alizokabidhiwa namba 1 wao wa chama kisiri siri, zinaweza kutibua plan yake ya kushika unamba 1 wa chama, kwani namba 1 aliepo anaweza kutumia cheo chake, na pesa hizo (Lisu anadai zilitoka kwa mama Abdul) kuendelea kubaki kitini kwa miaka mingine mi5 ijayo. Hivyo ndugu Lisu akaendelea kuwa anadhibitiwa na watoa pesa hao kupitia makubaliano waliyopanga kati ya mkuu wa wakuu na namba 1 wa chama chao.
So kwa hali ilivyo ni ngumu mno kwa mzee Lisu kuwaangusha ndege hao, kwani wameshajipanga kwa pamoja kuhakikisha jamaa anakuwa debe tupu. Yani apewe uwanja wa kupiga kelele na kubwawaja apendavyo ila mwisho wa siku wamchinjie baharini. I mean hatopata unamba 1 wa chama chake, wala ule ukuu wa wakuu. Ataachwa aendelee tu kubwabwa na kupozwa na cheo cha ukatibu mkuu wa chama.
Ndomaana mpaka leo si namba 1 wa chama chake, wala mkuu wa wakuu aliejitokeza kumjibu anayoongea. Cause wanajua ni mbio za sakafuni tu zitakazoishia ukingoni.