Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Gazeti kongwe la RAIA MWEMA ni kwamba aliyekua mkuu wa Wilaya ya Hai bwana Ole Sabaya anaogelea kwenye mabilioni ya shilingi.
Kazipataje hizi pesa wakati yeye ni mwajiriwa wa serikali? Ni biashara gani ya wazi Sabaya anafanya tusaidiane?
Eti mnaita huyo ndio Sokoine mpya, kuna watu hamliheshimu taifa kabisa. Endelee kumchukia Man kwa maamuzi yake kufurusha Manyang'anyi na majambazi yanayotumia madaraka yao kunitajirisha lakini Mama harudi nyuma.
MKUU wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro aliyesimamishwa kazi, Lengai ole Sabaya, ‘anaogelea kwenye utajiri wa mabilioni ya shilingi’, Raia Mwema imeelezwa.
Taarifa kutoka wilayani Hai, Arusha na Dar es Salaam, zinasema Sabaya anaweza kuwa mmoja wa wakuu wa wilaya wachache nchini, ambao wanamiliki mabilioni ya shilingi, yaliyotokana na madaraka aliyokabidhiwa. Kwa mujibu wa taarifa hizo, baada ya kufariki dunia kwa aliyekuwa Rais, Dk John Magufuli, Mkuu huyo wa Wilaya, alikutwa akimiliki zaidi ya Sh bilioni 3.
Mamilioni hayo ya shilingi, yalikutwa na vyombo vya usalama yamehifadhiwa nyumbani kwa Mkuu huyo mwenye makeke, wilayani Hai.
“Ninakwambia hivi, huyu bwana mdogo (Sabaya), anaweza kuwa amekusanya mabilioni ya shilingi, kupitia madaraka yake. Mapema mwezi uliopita, alikutwa na fedha nyingi nyumbani kwake, kutokana na ukaguzi maalumu wa vyombo vya usalama,” alieleza mtoa taarifa wa gazeti hili, kwa masharti ya kutotajwa gazetini.
Alisema ukaguzi huo, ulifanyika siku chache baada ya Dk. Magufuli kufariki dunia Machi 17 mwaka huu. Kupatikana kwa taarifa kuwa Sabaya anaogelea kwenye utajiri wa mabilioni ya shilingi, kulikuja siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kumsimamisha kazi juzi, kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.
Hata hivyo, Taarifa ya Ikulu juzi, haikusema Sabaya anachunguzwa kwa makosa gani, ingawa katika siku za karibuni, kuliibuka rundo la malalamiko dhidi yake, ikiwamo madai ya matumizi mabaya ya madaraka, rushwa, ukiukaji wa haki za binadamu, utekaji na utesaji. Aidha, kupatikana kwa tuhuma hizi, kumekuja wiki moja, baada ya Sabaya kufanya mahojiano na kituo kimoja cha utangazaji Dar es Salaam, akikana madai ya kupora fedha na mali za wafanyabiashara wakubwa mkoani Kilimanjaro na Arusha.
Tuhuma dhidi ya Sabaya zimekuwapo tangu enzi za utawala wa Rais Magufuli, lakini hakuchukuliwa hatua, kwa madai kuwa alikuwa akimlinda. Sabaya mwenyewe alikiri kuwa Rais Magufuli, mbali na kuwa Rais, alikuwa kama baba yake. Alisema, “nilikuwa na uwezo wa kumpigia simu hadi saa nane usiku na akipokea.
Kuna wakati nilikuwa natamani kupumzika na kazi hii ya ukuu wa wilaya, lakini Rais Magufuli alikuwa ananiambia ‘songa mbele niko nyuma yako’.” Mbali na madai ya kukiuka haki za binadamu, Sabaya anatuhumiwa kupokea rushwa, kwa njia ya vitisho kutoka kwa wawekezaji mbalimbali, akiwamo Cuthbert Swai, Mkurugenzi wa hoteli ya kitalii, Weruweru River Lodge.
Anatuhumiwa pia kutumia madaraka yake, kudai na kupokea rushwa ya Sh. milioni 10 kutoka kwa mfanyabiashara huyo, ikiwa mwendelezo wa tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na wawekezaji wengine wilayani Hai. Cuthbert alieleza kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo kadhaa na Sabaya, ikiwamo kuombwa rushwa ya kati ya shilingi milioni tano na milioni mbili.
Aidha, pamoja na kutoa mamilioni hayo ya shilingi, Cuthbert aliamriwa ndani ya saa 48 kuhamisha akaunti za hoteli ya Weruweru River Lodge, kutoka Moshi mjini kwenda Hai. Swai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Ahsante Tours, aliwahi kueleza mbele ya Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msafiri Mbibo, kwamba Sabaya amekuwa akitumia madaraka yake, kunyanyasa wafanyabiashara.
Alitoa tuhuma hizo, katika moja ya mikutano ya wafanyabiashara na TRA uliofanyika Moshi Julai mwaka jana. Alisema, kwa nyakati tofauti kati ya Novemba mwaka juzi na Julai mwaka jana, Sabaya alipokea Sh. milioni 10 kutoka kwake, fedha ambazo alizitoa kutokana na vitisho alivyokuwa akipewa na mkuu huyo wa wilaya. “Sabaya Novemba mwaka jana alinipa saa 48 kuhamisha akaunti zangu za Weruweru River Lodge na kuzipeleka Hai.
Nilifanya hivyo, lakini mpaka sasa sijui ni kwa nini. “Wakati huo huo, akawa anadai ushuru wa hoteli, ambayo yeye hajui kama ukiwa unalipa VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani) hutakiwi kulipa ushuru huo, unachotakiwa ni kulipa ushuru wa huduma,” alieleza.
“Mheshimiwa hicho kitendo hakukielewa, ilituchukua sisi wiki tatu nikihudhuria, kuanzia asubuhi mpaka saa nane bila kujali kuhusu wateja wangu,” alidai mfanyabiashara huyo. Aliongeza: “Nikamwambia sina, lakini baada ya vitisho vya mara kwa mara, wafanyabiashara wenzanu waliniambia nimpe tu, nisicheze na mjinga kwani atanitoboa jicho, hivyo nikampa kwa shingo upande.” Alisema: “Baada ya miezi michache, Sabaya alimiambia kuna kazi maalumu amepewa, ambayo inatakiwa fedha nyingi kuitekeleza. “Kwa hiyo, aliniambia wafanyabiashara wote wanatakiwa wachangie, hivyo akanitaka nitoe Sh. milioni 15.
Nikamwambia, biashara ya utalii imeyumba, hivyo siwezi kupata fedha hizo. “Hapo akatangaza uhasama na mimi. Akaenda kwenye mashamba yangu ya Rundugai, akasema nilidhulumu wanakijiji. Akatengeneza wazee bandia waliojifanya wamedhulumiwa, akatangaza kuyataifisha,” alidai Cuthbert. Mtoa taarifa alisema: “Huyu ni mmoja.
Lakini kuna watu wengi wameumizwa na Sabaya, na bado hawajawa na ujasiri wa kueleza haya hadharani. Nakwambia hivi, tujiandae kumkuta Sabaya akifikishwa mahakamani.” Alisema: “Muda wowote tutamwona Sabaya kwenye karandinga, maana aliyekuwa akimwabudu, kumlinda na kumpa kiburi, hayupo tena.” Mbali na madai hayo, Sabaya aliwahi kumtuhumu mfanyabiashara huyo, kuwa anaendesha shughuli za ufugaji wa wanyama wakiwamo nyoka, bila vibali kutoka mamlaka husika.
Kwa mujibu wa nyaraka ambazo gazeti hili linazo, Juni 11 mwaka jana, Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Hai, S. Kundya, alitoa kibali cha miezi sita kwa Weruweru River Lodge, kufanya maonesha ya ngoma za asili za kabila la Wasukuma na ya nyoka kwenye hoteli hiyo.
Katika barua yake, iliyobeba kichwa cha maneno: “Kwa yeyote anayehusika, Yah: kibali cha kufanya maonesho ya ngoma za asili za Kisukuma na maonesho ya nyoka, Kampuni ya Weruweru River Lodge kuanzia 11/6/2018 hadi 31/12/2018, saa nane mchana mpaka saa tatu usiku, siku za maonesho,” ofisa huyo alisema, Serikali imeruhusu kufanyika kwa maonesho hayo.
Hata hivyo, wakati kibali hicho kikibakiza mwezi mmoja kwisha muda wake, Swai alilalamika kupewa vitisho na Mkuu huyo wa Wilaya, na kulazimishwa kuandika barua ya kukiri kufuga nyoka bila kibali, agizo ambalo alilitekeleza Novemba 5 mwaka jana. “Nyoka hawakuwa mali yangu, bali ya Bwana Maganga kutoka Nzega, ambaye sasa ameshawachukua na kuwarudisha Nzega,” ilieleza barua ya Cuthbert kwenda kwa Sabaya. Vilevile, gazeti hili liliona leseni ya biashara ya nyara iliyotolewa na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), kituo cha Arusha yenye Na. 07064 ya Januari 19, ambayo ilitolewa kwa Shamba la Kikavu na kulipiwa ada ya Sh. 118,000.
Mwandishi wa habari hizi, alimtafuta Sabaya, kuzungumzia uhuma hizi na hatua ya Rais Samia kumsimamisha kazi. Lakini mara zote simu yake ilikuwa inaita bila kupokewa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, ambaye aliwahi kueleza kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ilipanga kumhoji Sabaya juu ya tuhuma za rushwa ambazo alidai malalamiko yake yamekuwa mengi, naye aligoma kutoa maoni yake. Alisema: “Namwachia Rais afanye kazi yake.
Sina la kusema kuhusu Sabaya kwa sasa.” Mghwira aliwahi kunukuliwa akisema, tuhuma zilizoanikwa na wafanyabiashara mkoani kwake kuhusu Sabaya, ni nyingi na hivyo ni lazima ahojiwe, na akaenda mbali zaidi akitaka kufanyika kwa kikao cha pamoja na wafanyabiashara.
Machi mwaka jana, Rais Magufuli alimtuma aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. Phillip Mpango na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angela Kairuki, wilayani Hai, kutafuta ukweli juu ya malalamiko ya wawekezaji dhidi ya Sabaya, ikiwamo kuwaweka ndani kwa saa 48.
Mbali na kuwekwa ndani, wawekezaji walikuwa wakilalamikia vitendo vya kudaiwa rushwa, au kuwekwa katika mazingira ya kudaiwa rushwa na Mkuu huyo wa Wilaya.
Chanzo: Raia Mwema