Pre GE2025 DSM Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
2,498
7,065
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ukweli mchungu Ila hizi timu zinawafanya Watanzania kuzidi kuwa wajinga

Hakuna tofauti ya mtanzania mwenye degree na ambaye hajui kusoma

Kuna siku nilikuwa nabishana jamaa mmoja namwambia hizi timu CCM anazitumia kutawala bila usumbufu!!

90% ya mashabiki wa hizi timu ni wajinga

Juzi tena Kuna mfanyakazi wangu anaomba ruhusa kwa mkuu wake eti akaangalie mechi ya Simba na almasry nilicheka Sana yaani uondoke kazini muda wa kazi kisa kwenda kwenye mpira?

Huu ukweli Lema kaongea hizi timu zingefutika au kuacha kubebwa soka la Tanzania lingeenda mbali Sana!!

Uchawa wote uanzia kwenye hizi timu
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

View attachment 3307480
Siasa sio sababu ya kutokufurahia vitu vingine, lema amezingua asipangie watu nini cha kufanya.

Jamaa ni siasa kali sana, suala watu kusapoti mabadiliko wanaweza kusapoti na huku wanashabikia mipira.

Lema aache siasa za kijuha
 
Hauwezi ukashabikia mpira halafu ukawa na akili timamu.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

View attachment 3307480
Mimi ni CCM akili haina itikadi Godbless yuko sahihi
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

View attachment 3307480
Kila siku mnasema watanzania wote wanafurahia na kutekeleza NR NE, Sasa watanzania gani ambao hawafuatilii Mambo ya chadema?
 
Namkubali sana Lema ila hapa amekosea kiasi fulani.
Mpira umewapa ajira watu wengi tu kuanzia wachezaji coaching team, management, wajasiriamali wa kwenye matukio ya mpira na wauzaji wa bidhaa za club husika, watu wa vyombo vya habari, n.k.
Bila hamasa na huo ushabiki kusingepatikana hizo faida.
Watu wanapenda kupata furaha na ushabiki wa hizo timu huwapa furaha.
Kama unakula, unavaa, unahitaji furaha japo kwa jambo dogo.
Huwezi kuita mpira vitu vya kijinga au kitu kisicho muhimu.

Kwa upande wa pili wanaona siasa inawanufaisha moja kwa moja watu wachache ambao ni wanasiasa.
Siasa ukiweka sana hamasa kuna uwezekano wa kujikuta jela, kupata ulemavu, kuuwawa, kupotea au kufilisika. Mfano Ben Saa8, Soka, Mawazo, na wengineo.

Sasa mtu anaona ajiweke kwenye hatari yote hiyo kwa manufaa ya nani?
Si bora aende kwenye furaha kwenye mpira?
Lakini ukiangalia kwa undani kwenye siasa unaweza kuhamasika au kuhamasisha ukaleta maendeleo makubwa kwa jamii yako na uzao wako ujao.
Siasa inahitaji Martyrdom (kujitoa muhanga) au sacrifice (kujitoa sadaka).
Mfano anayopitia Lissu au yaliyo wakuta akina Patrice Lumumba, Martin Luther King Jr, Che Guavara, Malcolm X, au akina Ben na Soka.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

View attachment 3307480
Lema sasa anaingilia vitu vya watu ,sasa unavyosema mpira ufutwe je ajira hizo zilizotokana na mpira zitasaidiwa na Chadema? Kuna wengin nao siasa hawazipendi wanaomba vyama vyote vifutiliwe mbali.

Tuheshimu haki za watu ,kila mtu ana haki ya kupenda atakacho ili mradi asivunje sheria.
 
Back
Top Bottom