Wakuu,
Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Jumatano, Novemba 27, 2024 nchini Tanzania, jijini Arusha kumekuwa na malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa, hususan CHADEMA
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mawakala wa chama hicho wamekusanyika nje ya ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha wakilalamikia kile walichokiita hujuma dhidi yao, baada ya kudai kunyimwa nakala za viapo vyao licha ya kuapishwa.
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, akiwaongoza mawakala hao, ameeleza kuwa kitendo cha kunyimwa nakala za viapo ni njama za mapema zinazolenga kuhujumu uchaguzi. Akizungumza kwa hasira nje ya ofisi hizo, Lema alisema: "Hapa hatuondoki, na kama wanataka kutuua waanze na mimi."
Lema amebainisha kuwa bila nakala hizo mawakala wa chama chao hawataweza kuingia katika vituo vya kupigia kura kesho kwa ajili ya kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi, hali ambayo amesema inalenga kuharibu uwazi wa uchaguzi huo.
Kwa upande mwingine, msemaji wa Jiji la Arusha, Ali Nyambi, amekanusha madai hayo na kueleza kuwa maandalizi ya uchaguzi yanaendelea vizuri. Nyambi amesema mawakala wa vyama mbalimbali tayari wameshakula viapo, isipokuwa mawakala wa vyama viwili waliokuwa bado. Amesisitiza kuwa kabla siku kuisha, mawakala wa vyama vyote watakuwa wamekamilisha zoezi hilo.
Malalamiko haya yameibua taharuki ya kisiasa, huku wananchi wakisubiri kwa hamu kuona jinsi uchaguzi utakavyoendeshwa katika maeneo yote. Uchaguzi huu unatarajiwa kuwa wa muhimu katika ngazi za mitaa na vijiji kwa kuwapata viongozi watakaohusika moja kwa moja na maendeleo ya kijamii.