Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,071
- 121,511
Wiki jana kitabu cha mwandishi Erick Kabendera kinachomhusu Rais Magufuli ndo kilikuwa habari ya mujini, at least humu kwenye viuchochoro vya kwenye mtandao.
Kitabu chake hicho kina madai makubwa sana ambayo hayakuambatana na ushahidi/ ithibati madhubuti.
Ni madai ambayo mtu unategemea kuyakuta kwenye kwenye machapisho ya udaku [tabloids].
Madai ambayo kwa kweli yametoa changamoto kubwa sana kwa watu kama mimi ambao hupenda kutumia common sense katika kutafakari na kutathmini mambo.
Unaposema eti Rais Magufuli alimuibukia makamu wake ambaye ndo Rais wa sasa, akiwa kavaa nguo za kulalia na akataka kumbaka, mtu yeyote mwenye akili anapaswa kuhoji. Siyo kumeza kama vile mtu huna hata akili moja!
Cha kushangaza, kuna watu wameyaamini kabisa madai hayo kuwa ndo ukweli wenyewe.
Wengi wa watu hawa wanasukumwa na hisia zao za chuki walizonazo dhidi ya Magufuli.
Hivyo, alichofanya Kabendera kwa kuyaandika hayo madai, ni kuzipa nguvu hizo hisia za watu hao walio na chuki kubwa dhidi ya Magufuli - confirmation bias.
Nimejaribu kufuatilia mapokezi ya watu ya hicho kitabu. Nilichokiona ni kwamba, gumzo la ujio wa hicho kitabu halijavuka mipaka ya mtandao.
Huku uraiani watu wala hawana muda nacho kabisa hicho kitabu.
Na mpaka sasa, kwa mujibu wa utafiti wangu huo usio rasmi, sijaona popote pale vyombo vya habari vya siku zote - magazeti, redio, na televisheni - vikijadili ujio wa hicho kitabu au hata kumfanyia mahojiano mwandishi wake.
Mahojiano pekee ambayo nayajua mpaka sasa, ni yale aliyoyafanya huko YouTube kwenye chaneli ya Gumzo la Ghassani.
Ni chaneli ndogo. Ina watu elfu 26 ambao wamejiunga nayo.
Na mahojiano aliyoyafanya mmiliki wa chaneli hiyo na mwandishi Kabendera, yametazamwa mara elfu 84 tu, tokea video hiyo ipandishwe kwenye chaneli mnamo tarehe 2, 2025.
Kwenye nchi yenye watu zaidi ya milioni 60, elfu 84 ni kiasi kidogo sana.
Sina takwimu, ila naamini vyombo vya habari vya siku zote hufikia idadi kubwa zaidi ya watu kuliko hao elfu 84 ambao wameitazama video hiyo huko YouTube.
Naona kitabu kimebuma. Vyombo vya habari vya Tanzania vimekipotezea.
Najua wapo wataodai kuwa vyombo vya habari vinaogopa kukizungumzia hicho kitabu kwa sababu zinazoeleweka.
Kwa kawaida, kwenye nchi zingine nilivyoona, mtu akiandika kitabu kumhusu mkuu wa nchi na atoe madai makubwa kiasi hicho, mwandishi huyo atatafutwa na kila chombo cha habari kufanya mazungumzo kuhusu alichokiandika.
Lakini kwa huyu Kabendera, hamna kitu. Si ajabu watu wa hivyo vyombo vya habari wamekisoma hicho kitabu na kuona ni jinsi gani ambavyo hakijajitosheleza na wakaamua kukipuuza tu.
Pia, hata waliotajwa nao wala hawajisumbua kujibu chochote kilichodaiwa na huyo mwandishi.
It’s a dud!