Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 5,876
- 13,708
Kwanza nilijiuliza kama huwa tunaandika nyuzi kwa watu tunao wapenda vipi kuhusu mwenzetu ambaye anapitia changamoto kwasasa,,nikaona niandike kwa ajili yako kipenzi
Kwanza Leejay49 nimesikitika sana kwa changamoto unazo pitia kwasasa najua vile unavyohisi na kama ulivyojieleza mwenyewe katika nyuzi zako kadhaa
Changamoto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu hivyo nawe ni mmoja wapo,wakati mwingine mungu anatupa majaribu ili kupima imani zetu je tutakuwa na subira au tutakufuru?
Inasemwa hivi imani ambayo haijajaribiwa basi si ya kutumainia,itajulikana una imani mbele ya mola wako endapo utashukuru kwa kila mapito unayopitia na bado ukaendelea kumwamini mola wako na huku unakuwa na subira, hatupewi majaribu sio kwakuwa hatupendwi na mola wetu ila kwakuwa majaribu ni sehemu ya maisha ya mwanadamu yoyote yule
Kuna aya katika quran Allah anasema "nitawajaribu kwa upungufu wa mali na watoto,kwa hofu,vifo.....kisha ikamalizia wape habari njema wenye kusubiri
Kwahiyo subira ni ibada kubwa sana, Nabii Ayubu salamu na amani ziwe juu yake aliumwa kwa miaka kumi na nane lakini siku zote alikuwa na subira, mwili ulitafunwa na maradhi akabaki na ulimi wenye kumtakasa mola wake na bado aliendelea kumsifu Allah, hakunung'unika bali aliamini ni Mola wake pekee mwenye suluhisho la maradhi yake
Hivyo nawe endelea kuwa na tumaini kwa Mola wako kuwa huyo aliyekupa mitihani ndiye pekee awezaye kuondoa maradhi yako, Mungu hakupi mtihani usio uweza bali anajua utauweza kikubwa amini katika ukuu wake na endelea kumwomba bila kuchoka
Wewe ni mwanamke shujaa na mwenye kujiamini utayapita mapito haya kwa ujasiri na nguvu kubwa,ni swala la mda tu utarudi katika afya yako tena na kuendelea katika majukumu yako ya kawaida
We love you
Ni hayo tu!