Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 339
- 705
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imepokea maombi ya kurejea nauli za mabasi yanayotoa huduma ya usafiri wa haraka kutoka kwa UDART ambayo inatoa huduma za mpito za usafiri wa Mabasi ya Haraka katika Jiji la Dar es Salaam
Mapendekezo ya Nauli yaliyotolewa ni kama ifuatavyo, Nauli ya Njia Kuu - Tsh. 1,000, Abiria wa Njia Lishi (Feeder Route) Tsh. 600, Njia ya Kimara - Kibaha Tsh. 1,200 na Nauli za Wanafunzi Tsh. 200
Mkutano huo utafanyika tarehe 03 Julai 2024 katika Ukumbi wa mikutano Arnaoutouglou, Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3.30 asubuhi. Kutokana na umuhimu wa mkutano huo, LATRA inawaalika wadau wa sekta ya barabara na wananchi kwa ujumla kushiriki bila kukosa katika mkutano huo muhimu.
Pia Soma