Kwanza muelewe siko na sijawahi kuwa weak namna hii ila huyu binti mzungu wa Kigoma nimempenda sana.
Kwa mwezi sasa nipo Kigoma mwisho wa reli, juzi katika shughuli zangu nikakutana na mwanamke ambaye ninaona ni wa maisha yangu, ni mzungu mbongo maana hata kilugha anaweza za waha wa Kigoma, she is so beautiful, local but international standard, kutoka rich family, mtu mwenye exposure kubwa ametembelea majiji makubwa duniani yani likizo hata ya wiki 2 anasafiri, shule kasoma hapa Tz.
Kanipenda japo nimemuacha kama 7 years kiumri, binafsi nimetembelea nchi kadhaa duniani wiki mpaka miezi 2, ila sijui ni uoga, kupenda ama nimelogwa ninamuogopa kinoma. Kesho nna date nae sijui ni nini kimenipata ameniambia atalala kwangu siku chache, kisha anaenda Dar.
Sijafanikiwa kumjua vizuri maana yeye ndo wa kwanza kunishobokea, alafu kwa mambo ya kazi tukitumiana text zinaweza ku range hata masaa mawili au uki call asiwe hewani, na mimi niko kwenye expedition areas ambazo hamna network mda mwingine.
Nina familia sijaoa, maana nina mtoto, mtoto na mama yake(mchumba) nimemchumbia official 2015 ambaye anajua sina mpango wa ndoa kabisa(nilimchumbia ili asisemwe sana na mama yake) na yeye hataki hata nimuoe wala kunizalia mtoto mwingine ila tupo pamoja Ijumaa (alikuwa) anakuja kwangu anaondoka Jpili, ila huyu mzungu ni komesha, sijaspend nae hata 30mins in person ila ninamuogopa na kumpenda pia.
Ninachowaomba dada zangu wapendwa mniambie ni mambo gani ya kufanya niwapo nae kesho mpaka atakapoondoka kumteka kisawa sawa, maana booking atafanya leo usiku sasa kama ni siku mbili tatu sijajua, ni kama akili yangu ime stuck ivi, ninaomba msijadili kuhusu mtoto na mama yake maana hamna ndoa na yeye hataki.