Habari za wakati huu ndugu na marafiki wapendwa wa Jamii Forums....
Ni siku nyingine tena tulivu ikiambatana na manyunyu ya hapa na hapa pale kwa sisi wakazi wa Dar......
Leo ningependa kuwashirikisha katika jambo muhimu sana ndugu zangu ambalo hata mimi binafsi ninaweza kuwa shahidi kabisa....
Kuna kipindi nyakati za nyuma kidogo nilitokea kumtamani binti fulani hivi ambaye tulikuwa tukiishi nae karibu na nilipokuwa nikiishi mimi...kusema ukweli huyu mimi sikumpenda isipokuww nilikuwa namuhitaji kwa ajili ya kukidhi matakwa yangu ya kimwili.....kutokana na ushawishi mkubwa nilifanikiwa kumnasa yule binti na tukaanza kushiriki ngono huku yeye akijua kuwa mimi ndiye mumewe mtarajiwa.....yule binti alikuwa ni binti mwenye kujitegemea maana alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni fulani kubwa hivi ya kigeni kwa hiyo suala kipato alikuwa tatizo kwake....alichokuwa anakihataji ni mapenzi au mume ambaye aliamini kuwa ameshampata.....
Baada ya kukidhi haja zangu nikaanza kumkwepa kwa maana nilimuona kama ni kero vile kwangu.....yule dada nilimpa wakati mgumu sana kwa mabadiliko yale....na alikuwa akilia mbele yangu mara kwa mara akinisihi nisimuache lakini mimi sikuelewa lolote lile....yule mwanamke akakata tamaa na akaamua kuachana na mimi lakini alinitamkia maneno mazito sana kuhusu maisha yangu....ambayo nilianza kuyaelewa maana yake baada ya mwezi kupita tangu kukata mawasiliano naye.......
Niliona ghafla mambo yangu yanabadilika na kuwa mabaya kabisa....biashara zangu nyingi sana zilikwama mpaka nikawa nakosa hata hela ya kula......ile hali ikanishtua sana maana haikuwa kawaida ikabidi kuahangaika katika mambo ya kiswahili ndipo wataalamu waliponifunulia kuwa kuna mtu ana kinyongo na wewe kwa hiyo unatakiwa ukamiombe msamaha maana ndio njia pekee ya wewe kuondokana na mikosi hiyo maana hakuna aliyeniroga.....
Ikanibidi kwa unyonge kabisa nijipendekeze kwa yule binti na kuanza kujenga naye ukaribu upya na kuomba misamaha mingi sana....
Baada ya muda nikaona mambo yanaanza kubadilika na kuwa kama kawaida.....
N:B Dhumuni la mimi kushare kisa hiki ni kuwaasa vijana kuwa kama mwanamke huna mipango naye ya muda mrefu basi usimpotezee muda wake bure maana utamuacha na sononeko ambalo litakuletea mikosi kwenye maisha yako.....wapo vijana wasomi wanaohangaika kutafuta kazi takribani miaka kumi....wapo vijana wanaojaribu kuanzisha biashara zao lakini huwa zinakufa.....wapo vijana wanaofukuzwa kazi katika mazingira ambayo hata yeye hawayaelewi...hizi ni moja ya athari za watu waliokuwa na vinyongo na wewe.....
Stuka kijana