La ukame wa mabwawa ya kufua umeme ni kama la kimbuga Job na tani tano za dawa za kulevya kukamatwa Mtwara

mwananyaso

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
2,995
3,399
Hii nchi imejaa usanii sana ,nakumbuka hawa mafisadi na wauza dawa za kulevya waliweza kupenya mpaka kwenye mamlaka ya hali ya hewa na kutangaza kimbuga JOB, kwa lengo la kuwatisha wavuvi na kuhakikisha wanaondoka baharini ili wapitishe gendo lao la tani tano za heroin.

Kiukweli si wavuvi si askari wa doria waliigopa bahari.

Wapo askari wa mtwara ambao walijua hii Inaweza kuwa mwanya kwa wahalifu ,wakawa standby,walifanikiwa kukamata hiyo shehena
Inasemekana askari aliekamata mzigo ule aliingia matatani, na mpaka leo ile kesi hatuiskii ikiunguruma ,na mzigo ule haijulikani ulikopotelea na hakuna anayehoji.

Haya ingekuwa Magufuli yu hai ingejulikana tu ni nani wamiliki wa kago ile.
 
Haya ingekuwa Magufuli yu hai ingejulikana tu ni nani wamiliki wa kago ile
Mbona mnamfanya JPM kuwa invicible? Mbona mafuta kule kigamboni yalikua yanapitishwa kimagendo imekuja kujulikana mwaka huu au JPM hakuona? Mbona uhalifu wa Sabaya ndio umekuja kujulikana mwaka huu ina maana wakati anapora Fedha JPM hakuwepo? Kipindi Nchambi anakutwa na silaha za ujangili na wanyama pori JPM hakuwepo? Ama Tanzanite zinavyopitishwa chini ya ukuta JPM alikua amekufa?

Hayo ya Jobo yalitangazwa na CNN au wauza madawa wana mtandao hadi CNN? Tupunguze conspirancy, cha msingi ungesema tu waliangalia fursa ila sio kusema kilikua kimbunga feki!!

Then umewahi kwenda tume ya kudhibiti dawa ya kulevya kuulizia hyo kesi ama kila siku unakesha kwenye blog za umbea tu unategemea habari serious utakutana nayo??

JPM alikua binadamu pia tusimfanye Mungu mtu, kikubwa ni kwamba alibana tu taarifa ila nakuhakikishia kuwa ufisadi haukuwahi kuisha.
 
Back
Top Bottom